MUSOMA
Baadhi ya Wagombea Ubunge kupitia Viti Maalum UWT Kundi la Wanawake wamelamikia kuwepo kwa mazingira ya Rushwa katika Uchaguzi uliomalizika jana.
Habari kutoka katika chanzo chetu cha habari zinadai kuwa baadhi ya wagombea waliokuwa madarakani walitoa fedha na kuwalaza wajumbe kabla ya Uchaguzi kinyume na taratibu, kanuni na Sheria iliyopitishwa huku baadhi yao wakinunulia wagombea vinywaji huku kura zikiendelea kupigwa kinyume na Kanuni za UWT za mwaka 2010.
Wakati kura zikihesabiwa taarifa kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi, Alhaji Kundya ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza alisema kuwa Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa (TAKUKURU) iliwakamata watu wawili ambao walikuwa wanahesabiana fedha.
Habari kutoka Mjini Musoma zinadai kuwa Taasisi hiyo ingefanya hivyo mapema ingefanikiwa kuwanasa wagombea wengi ambao kwa asilimia kubwa walitoa takrima.
Rushwa bado ni kikwazo katika jamii ya watanzania walio wengi kuwa inatoa fursa ya kuchagua kiongozi asiyefaa katika kuwatumika wananchi.
Katika Chumba cha kuhesabia kura Mgombea RoseMary Kirigini alibeza wagombea walioshindwa na kumwambia Mshindi wa tatu kuwa atamsaidia Dodoma katika kinyanga’anyiro cha Kapu.
Watu watano waliteuliwa na Kamati ya Baraza la Mkoa kusimamia kura huku kanuni ikiwaruhusu wagombea kuteua mtu wake ama kwenda mwenyewe,ambapo wengi wao walikwenda kusimamia kura zao.
Kundi la Wanawake kura zilizopigwa zilikuwa 437 ambapo wajumbe walitakiwa kuweka alama ya vyema kwa watu watano kwa kila karatasi iliyo na majina na wagombea.
Kura zilikuwa 437 zilizoharibika tano na halali zilikuwa 432.
Kwa mujibu wa taratibu za CCM hakuna ushindi huo uliopatatikana kwa wagombea si kigezo bali mpaka washindi kutoka wa wabunge wa majimbo yote Mkoa wa Mara wapite ndipo watakapotangazwa,endapo majimbo yote yatapitishwa wabunge wa CCM kuna uwezekano wa kuteua washindi watatu na watakaposhindwa kupita nafasi itabaki ya Mbunge Moja kwa Mkoa.
Kwa mujibu wa Ratiba ya mchakato wa kuwapta wagombea wa CCM wa Urais, Ubunge,Uwakilishi na udiwani katika uchaguzi Mkuu wa dola inasema baada ya Uchaguzi huo kuisha 30 Julai,Kamati za utekelezaji za UWT za Mikoa zinatoa mapendekezo kwa kamati za siasa za Mikoa.Agosti 2 Kamati za siasa za Mikoa litaandaa mapendekezo ya UWT Taifa.
Kwa upande wa ngazi ya Taifa Agosti 4 Baraza Kuu la UWT Taifa litaandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.
Matokeo ya kura aliyekuwa Naibu waziri wa Elimu ,Gaudentia Mgosi Kabaka aliibuika Mshindi kwa kupata kura 358 akifuatiwa na Rosemary Kirigini 288,wengine ni Agness Mathew 277,Kichena Chambiri 264,Nacy Msafiri 257,Rukia Wandwi, 214,Francis Stella Sana 96 ,Veronica Nyerere 62,Evelyne Warioba 63,Norah Mkami 62,Lucy Malegeri 76,Caroline Nyerere 50,Jane Ngabo 48,
Eva-Sweet Musiba ambaye ni Mwandishi wa habari vyombo vya CCM alipata kura 40 na Consolata Maganga alipata kura 24.
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema watu wawili ambao jana walikamatwa na Taasisi ya kuzuia rushwa katika Uchaguzi huo wamefikishwa Mahakamani na wamekosa dhamana badao haijajulikana ni Mgombea gani aliwapatia fedha hizo.