Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga akiteta jambo na Mhashamu Baba Askofu MKUU wa Chuo Kikuu cha Stella Maris( STEMMUCO) Norbet Mtega, mara baada ya kumaliza hotuba yake katika mahafali ya kwanza ya Chuo hicho.
MWENYEKITI wa Bodi ya Chuo
Kikuu kishiriki cha Stella Maris,Tawi
la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (STEMMUCO),Mhashamu, Gabriel Mmole
ameipongeza Serikali kupitia bodi ya mikopo
kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Chuo hicho.
Aliyasema hayo juzi
katika mahafali ya kwanza ya Chuo hicho ya kuhitimu Shahada ya kwanza ya
Sanaa/ualimu (Bachelor of Art with Education) wakati akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mahafali hayo yaliyofanyika
katika viwanja wa Chuo Mjini Mtwara.
Alisema anaishukuru Serikali kwani bila wao pasingekuwepo na
mafanikio yoyote ya Chuo kwani ukubaliwa wao wa kutoa mikopo kwa Chuo hicho
ndio umesababisha mafanikio katika kufanikisha wanachuo kumaliza masomo yao vyema.
“Natoa pongezi za dhati kwa serikali ya awamu ya nne ambayo
imetuwezesha kutoa mikopo kwa wanafunzi wetu bila kubagua itikadi za dini
ukizingatia kuwa sisi ni taasisi ya dini,bila wao tusingefanikiwa”. Alisema
Mhashamu Baba Askofu Mmole.
Akifungua Mahafali hayo ya kwanza ambayo yalianza kwa
maandamano, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga alisema ukosefu wa ajira kwa vijana walio wengi
unatokana na baadhi ya wahitimu wa Vyuo Vikuu kutotaka ama kutoweza kuchukua
masomo ya Sayansi na hisabati, pia fani ya ualimu ambazo zina fursa ya ajira.
Alisema kuwa tatizo la wahitimu wa Vyuo Vikuu kurudisha
mikopo waliokopeshwa bado ni kubwa, ambapo kufikia Juni 2012, madeni ya
wahitimu wa Vyuo Vikuu yakiyokuwa yameiva yalikuwa Bilioni 160.7 na kati yake,
Sh Bilioni 39.5 zilitakiwa ziwe zimeishakusanywa kutoka kwa waliokopa lakini
asilimia 49 tu kati ya hizo zilikuwa zimekusanywa na bodi ya mikopo ya wanafunzi.
Aidha ametoa wito kwa Vyuo vya elimu ya juu kurekebisha
kasoro zilizopo kwa kutilia maanani masomo ya Hisabati na Sayansi na
kuhakikisha kila fani au program katika vyuo vikuu vyote kunakuwepo na masomo
ya ujasilimali (Bachelor of Business Administration/Management in Entrepreneurship)
ili kuwaandaa wahitimu kujiajiri kama hawatapata kazi za
kuajiriwa.
Alitoa wito kwa wahitimu kuwa tayari kufanya kazi popote
bila kubagua maeneo kama kama wengi wao wanavyopenda Mijini.
Katika awamu ya nne ya Serikali kutoka mwaka 2005/2006-2011/2012,
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo Iliyoundwa mwaka 2005, ilikopesha wanafunzi
480,472 jumla ya Sh. Trioni 1,133,386,869,000
ambapo Chuo hicho kimefaidika n amikopo hiyo ambapo asilimia 94 ya wahitimu,pia
imetoa ekari 140 kwa ajili ya mendeleo ya Chuo hicho,ambapo jumla ya wahitimu (kifungua
mimba) wapatao 1,100 wamehitimu.
Naye Mhitimu katika Chuo hicho, Wini Israel Musiba aliishukuru
Serikali kwa kutoa mikopo hiyo na kwamba
inajali familia duni si kama awali
ambapo jamii ilidhani mikopo ni kwa
watoto wa wakubwa peke yao,pia alitoa wito kwa Serikali kuweka miundo
mbinu ya barabara na Umeme ili walimu wafanya kazi zao kwa umakini zaidi kwa kuzingatia masomo ya sayansi yanayohitaji
maabara zenye Umeme hasa vijijini.
No comments:
Post a Comment