Wednesday, December 12, 2012

POLISI YAENDELEA NA UCHUNGUZI TPA

DAR ES SALAAM POLISI inaendelea na uchunguzi wa watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutaka kutoa malori 22 kwa kukwepa ushuru wa mamilioni bandarini, huku ikiwasaka watuhumiwa wengine waliohusika katika mchakato huo. Akizungumza na Uhuru,kamanda wa polisi wa Bandari, Fotnatus Muslimu alisema kuwa kuwa tuhuma wazaotuhumiwa watumishi hao ni za kughushi nyaraka linahitaji uchunguzi wa kina na watakapokamilisha jalada litapelekwa kwa DPP kwa ajili ya kupangiwa mashitaka. Watumiwa hao ambao wapo nje kwa dhamana kwa upande wa TPA kitengo cha mapato, Mary-Stella Minja, Amir Mshegama, Kennedy Kessy na Gladyness Magerere na Andrew Masaga ambaye ni mfanyakazi wa TRA na Antipas Otieno, kutoka kampuni ya Multi Model. Kamanda Muslimu alisema kwa sasa wanaendesha msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika mchakato huo wa kughushi nyaraka na upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa ajili ya kutoa maamuzi. Watumishi hao walitiwa mbaroni hivi karibuni wakituhumiwa kuhusika na mtandao wa kutoa malori 22 yaliyoingia nchini mwaka 2010 yaliyopaswa kulipiwa ushuru wa bandari wa sh. milioni 616 ambapo wao wanadaiwa kubadilisha nyaraka na kuonyesha maroli hayo yaliingia nchini mwaka 2012. Kwa mujibu wa taarifa hizo wakati wakitoa mzigo huo ambao nimali ya Kampuni ya Dhandoo a mjini Mbeya, nyaraka zilibainika kuwa ni za kughushi na kuna ukwepaji wa sh.milioni 600, kwani badala ya kuonyesha sh.milioni 616 nyaraka zilionyesha sh. milioni 16. Kutokana na hilo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Injinia Kipande Madeni alisema matukio ya wizi na uhujumu wa mapato ya serikali ni makubwa na yanasababishwa na wafanyakazi wasio waaminifu wa TPA, TRA na kampuni za upakuaji na upakiaji mizigo bandarini. Akizungumzia tukio hilo, Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe, alisema bandari ya Dar es Salaam imekuwa na sifa mbaya ya wizi wa mizigo na hivyo kuchafua jina la Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki zinazotumia bandari hiyo, hivyo ni lazima isafishwe ili vitendo vya udokozi viwe historia.

No comments:

Post a Comment