Tuesday, December 18, 2012
WAFANYAKAZI KOTE NCHINI KUFANYA MGOMO
SHIRIKISHO la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limesema kuwa endapo Serikali haitapandisha mishahara ya wafanyakazi kama ilivyopangwa wataamua vinginevyo na kwamba wanaitaka itangaze kima cha chini cha mshahara na marupurupu kwa sekta binafsi kabla ya April 2013.
Rais wa Shirikisho hilo, Omary Juma amewaambia waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam Asubuhi.
Alisema kuwa Kamati ya Utendaji ya Shirikiswho hilo, katika kikao chake cha Desemba 13-14 mwaka huu Mkoani Morogoro pamoja na mambo mengine kilijadili kwa kina, hali ya mazingira ya kazi nchini na kushuhudia kuwepo kwa mazingira magumu ya kazi na yalidumu kwa kipindi kirefu bila ya kupatiwa ufumbuzi.
Ameiomba Serikali katika bajeti yake ya mwaka 2013/2014 ilenge kuongeza kima cha chini cha mishahara kwa sekta ya Umma kwa asilimia 100,kupunguza kodi ya mapato ya ajira hadi kiwango kisichozidi asilimia 11,kwani ni hatua ya awali ya kuwezesha mfanyakazi kukabiliana na ongezeko kubwa la mfumko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha.
"Kwa tarbani miaka saba iliyopita, Serikali imekuwa ikitoa ahadi ya kubotresha mashlahi ya wafanyakazi lakini hadi leo hii hali za maisha ya wafanyakzi walio wengi ni duni, huku wakishudua watanzania wenzao wachache wakizidi kuneemeka na kuwa na utajiri wa kupindukia"Alisema Juma.
Aliongeza kuwa hadi sasa wafanyakazi walio wengi wenye mishahara ya kati ya Sh.70,000-100,000 wanaishi kwa Sh.3,000-4000 kwa mwezi na ndio walio wengi hasa katika sekta binafsi,hali kadhalika katika sekta ya Umma ambapo mtumishi wa chini analipwa sh.5,700 kwa siku na sh.170,000 kabla ya makato huku kodi kubwa kwa mfanyakazi ikikatwa pia kuwepo kwa ongezeko la wageni wanofanya kazi nchini kinyume cha sheria.
Aidha ameitaka Serikali pia kupunguza kodi kwa wafanyakazi kutokana na makato wanayokatwa wafanyakazi ambapo wafanyakazi wanakatwa kodi kwa asilimia 46 huku wawekezaji na wafanyabishara wakubwa wakilipia wasatani wa asilimia 24 tu.
"Utakuta mfanyabiashara anauza bidhaa zake,kwa kufuatilia soko kuu na lenye faida liko wapi, na akijipenyeza kidogo anaweza asilipe kodi na akishakamatwa anasema amekosea analipa kodi huku akijua amepata faida kubwa, sasa mfanyakazi aliye kwenye pay Roll' hawezi kukwepa kodi au kulipa deni chini ya kiwango kwa kuwa hauwezi kukimbia"Alisema Juma.
Kamati hiyo pia iliangalia hali ya ukosefu wa ajira nchini na kubaini kuwa hali sio nzuri kutokana na ongezeko kubwa la shukle na vyuo a,balo haliendani na ongezeko la vyanzo vya ajira na kwamba vijana wengi wanakwepa sekta ya Kilimo ambayo ndio yenye uwezo mkubwa wa kubeba sehemu kubwa ya ajira lakini kutokana na miundo mbinu isiyoridhisha wengi wao hukimbilia mijini.
Alisema kuwa mahusiano baina ya shirikisho na Serikali yataendelezwa pale madai ya wafanyakazi yatakapotekelezwa kwa muda mwafaka na maboresho ya Pensheni yalenge kuhakikisha kuwa kikokotoo kizuri cha Pensheni kilichop hivi sasa 1.540 ndicho kitakachopotishwa kwa mifuko yote na kwamba wafanyakazi hawatakuwa tayari kuona kikokotoo kingine kikubwa zaidi ya hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment