KILWA MASOKO.
WAKAZI wa kijiji cha Nangurukuru,kata
ya Kisingino,Wilaya ya Kilwa wameiomba Serikali kukamilisha zahanati ya Kijiji
hicho ili waondokane na hadha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo muhimu.
Katibu wa Ujenzi wa Zahanati hiyo,Rashid Changa
alisema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwaka 2007, na mpaka sasa iko
katika hatua za mwisho za upigaji bati na
baada ya hapo Serikali inapaswa kukamilisha ujenzi huo.
Jiwe la Msingi la Zahanati hiyo liliwekwa na Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Rais Utawala Bora George Mkuchika ,Machi 25 2011 ambapo ilitolewa
ahadi ya kuchangia kukamilisha ujenzi huo kiasi cha Sh.Milioni 40,kutoka kwa
Daktari wa Wilaya,Mike Mabimbi kwa ajili ya kumalizia jengo hilo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nangurukuru,Shaibu Mmula
alisema kuwa zahanati hiyo kwa sasa imeanza kuweka nyufa kutoka na kukaa kwa
muda mrefu na hivyo inaweza kuigharimu
serikali pamoja na wananchi fedha nyingi za ujenzi mpya endapo itabomoka.
Alisema kuwa wananchi wamechangia nguvu zao kiasi cha Sh.
Milioni 34 na Halmashauri kupitia mfuko wa jimbo imechangia Sh Milioni 1.5 .
Kwa upande wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu idadi na ongezeko la wanachama ni
hafifu kutokana na changamoto zinazoikabili Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na zahanati,soko
na stend, huduma ya maji.
Aidha Katibu Mwenezi wa tawi la Nangurukuru,Said matale alisema
endapo changamoto hizo zitapata utatuzi,hakuna chama chochote kinaweza kushinda uchaguzi Mkuu 2015
na ametoa wito kwa Serikali kuangalia uwezekano wa kuchimbiwa malambo hasa
katika maeneo ya Kwakumtoni, Karasha, Dodomezi na Lingaula.
Aliongeza pia kuwa kumekuwa na unyanyasaji kwa upande wa
wavuvi kubaguliwa kiitikadi na kwamba kama wewe si mwanachama wa Chama cha CUF
uwezi kuvua samaki katika Bahari,hiyo
ambapo tatizo hilo linaonekana kuwa sugu kwa upange wa Kilwa Kivinje.
No comments:
Post a Comment