Monday, December 17, 2012

MBUNGE VICENT NYERERE ASEMA KAMPENI MENEJA ALIYEHAMIA CCM HAJAWAHI KUMFANYIA KAMPENI.

Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Mara,kimepata pigo mara baada ya kuondokewa na kamepni meneja wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vicent Kiboko Nyerere mara baada ya kurejesha kadi na kurejea CCM. Inadaiwa kuwa Kampeni Meneja wa Mh. Mbunge, Nyerere alikuwa Juma Songo,lakini Mh Vicent mwenyewe amemkana na kusema kuwa hajawahi kuwa Meneja Kampeni wake ila Chama kimefanya kile alichokiita hiyo ndo Siasa. Hata hivyo katika ziara hiyo ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, alidiriki kuwafukuza waandishi wa habari wakati wa tadhimini ya uchaguzi iliyofanyika katika ofisi za CCM Mkoa huku akiwaacha waandishi wake wa habari ambao alikwenda nao kwenda ziara yake Mkoa wa Mara. Kitendo cha Mwenyekiti huyo kuwafukuza kinadharirisha taaluma ya habari,hasa kwa waandishi walioko Mikoani kuonekana hawafai,huku wakifanya kazui kila siku. Taasisi zinazohusika na haki kwa waandishi na vyombo vya habari iliangalie kwa kila,na maelekezo yatolewe kwa ajili ya hili. Huu ni udhalilishaji mkubwa ambao Kiongozi wa Juu kama Mwenyekiti wa wazazi Taifa, Abdallah Majura Bulembo ambaye aliwahi kuwa Diwani katika Kata ya Nyasho kufanya udhalilishaji huu.

No comments:

Post a Comment