Thursday, December 6, 2012

KITABU CHA PICHA MAHAFALI YA KWANZA YA SHAHADA YA SANAA NA ELIMU(STEMMUCO)




Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu wakisubiri kutunukia Shahada yao katika mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Mtakatifu AugustinoTawi la Mtwara (STEMMUCO),





Mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki,Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Milton Makongoro Mahanga akiwa na Mkuu wa Chuo cha Stella Maris Mtwara (STEMMUCO),Mhashamu Baba Askofu Mkuu,Norbet Mtega,akishiriki maandamano ya wanataaluma kuelekea viwanja vya Chuo kwa ajili ya kuwatunuku Shahada wahitimu.





Mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki,Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Milton Makongoro Mahanga akiwa na Mkuu wa Chuo cha Stella Maris Mtwara (STEMMUCO),Mhashamu Baba Askofu Mkuu,Norbet Mtega, mara baada ya maandamano kabla ya kuwatunuku Shahada ya kwanza wahitimu wa Shahada ya Sanaa na Elimu,katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustion Tawi la Mtwara juzi.


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia sherehe hiyo ambayo kwa wao haikuwa vyema kwani hawakuwa na maandalizi yoyote ya viti kwa ajili ya kuandika habari wakiwa wamekaa kwenye viti, waandishi wa print Media wanapaswa kuwa wanaandaliwa sehemu yao ya kukaa kuliko kuwatelekeza, huku hotuba zao zikijaa shukrani nyingi kwao, bila ya kuwajali, ni muda mwafaka sasa, taasisi zote zianze kuwajali wanataaluma hao ambao ni kiungo muhimu si kwa Serikali tu bali hata mashirika kama ya dini n.k.

MKUU WA CHUO akifurahi jambo na Mgeni rasmi,anaonekana kusema sherehe imekwenda MZUKA ETI EH!!!


Mgeni rasmi katika Mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu Kishiriki,cha Mtakatifu Agustino,Stella Maris Mtwara( (STEMMUCO) Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Milton Makongoro Mahanga. akimpongeza mmoja wa wahitimu wa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Elimu,Wini Musiba,mara baada ya kutunukiwa.

No comments:

Post a Comment