Tuesday, December 18, 2012

BARAZA LA WAGANGA WA TIBA ASILIA LIMEITAKA TFDA KUCHUNGUZA MAKAMPUNI ZA MADAWA(VIRUTUBISHO KUTOKA NJE YA NCHI.

BARAZA la Waganga wa Tiba Asilia (BAWATA) limeitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kudhibitisha madawa yanayoingizwa nchini na kuuzwa kwa gharama kubwa kama madawa na virutubisho. Katibu wa Baraza hilo, Shariff Karama amesema leo asubuhi katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo Jijini Dar es Salaam,alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Aliyasema hayo baada ya kuulizwa swali na Uhuru,kutokana na kuwepo msukumo hafifu wa tiba za asili kutoka nchini kwetu na badala yake kuingizwa virutubisho kutoka nje ya nchi na vyenye gharama za juu, huku vikiwepo dawa nzuri za asili kutoka Tanzania ambazo hazitumiwi na watanzania. Alisema kuwa kumekuwa na msukumo hafifu wa utumiaji wa dawa za asili zinazotengenezwa nchini na ambazo tayari zimedhibitishwa na mkemia mkuu wa Serikali jambo ambalo wananchi wengi wamekuwa wakienda kununua virutubisho visivyo kuwa na tiba ndani yake. Akizungumzia juu ya vibali vya waganga wa tiba asilia, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Shaka Shemuiwa alisema kuwa Serikali imekuwa ikisuasua kutoa vibali vya waganga wa tiba asilia ili waweze kusaidia watanzania wengi ambao hawana uwezo kumudu matibabu kwa gharama kubwa huku madawa ya magojwa sugu ya kisukari na Malaria yakiendelea kupoteza mamilioni ya watanzania. Aliiomba Serikali na jamii kwa ujumla kutenganisha waganga wa jadi na waganga wa Tiba asilia jambo ambalo linawezekana kwao kukosa kibali baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupiga marufuku waganga baada ya kukithiri kwa mauaji ya vikogwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) na Wizara ya afya kutilia msukumo kuhamasisha tiba asilia kwa mujibu wa sheria ya tiba asilia ya mwaka 2000. Alitaka pia jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokiuka sheria ya uvutaji sigara hadharani iliyopitishwa na bunge mwaka 1985 ambayo ina hadhari kubwa kwa asiyevuta kutoka na moshi wake kuwa na sumu aina ya Nicotyne ambayo inatengeneza sumu kali. "uwenda hata askari hawajui hii sheria kwani utakuta mtu anavuta sigara hadharani mbele yake lakini cha kushangaza anamwacha,lakini moshi huo una madhara makubwa".Alisema Shemuiwa. Aliongeza kuwa mabadiliko ya tabia nchi na hewa ya ukaa pia ni tatizo kubwa,hivyo amewataka wananchi kupanda miti ili kuboresha mazingira. Tanzania imejaliwa kuwa na hazina kubwa ya miti mingi ya asili ikiwemo Alovera, Moringa Tree,Mwarobaini,mibomo kaburi na mengineyo ambayo ni tiba nzuri kwa binadamu. Pia Tiba asilia ni tiba nzuri ambayo haina madhara makubwa kwa mtumiaji kuliko madawa mengine. Baadhi ya watafiti nikiwemo na mimi ambaye huwa situmii vidonge kwa ajili ya tiba nimegundua kuwa dawa hizi ni nzuri na hazina madhara mwilini. Serikali kupitia Wizara ya Afya utoe msukumo wa hali ya juu na uwekezaji wa tiba asili ambazo nchi kama China,zinatengeneza tiba asili kuwa vidonge na vinapoingia nchini vinauzwa kwa gharama kubwa kwa nini tusitengeneze wenyewe?

No comments:

Post a Comment