Monday, December 31, 2012

WAGENI KUTAMBULISHWA KWA WENYEVITI WA MITAA.

KATIKA kuhakikisha hali ya Ulinzi na Usalama inaimarika, katika manispaa ya Musoma, wananchi wa kata 13 za Wilaya ya Musoma wametakiwa kutoa taarifa za wageni wao kwa Wenyeviti wa Mitaa,Mkuu wa Wilaya ya Musoma,Jackson Msome,amewaambia wananchi wa kata za Nyakato,Bweri na Nyasho kwa nyakati tofauti kuhusu usalama wao na kuwatambua wageni wanaoingia majumbani kwao. kuhusu mauaji ya kutisha ya kukatwa watu vichwa yapo lakini idadi si iliyotajwa.na ni Wilaya jirani, Kumekuwa na makundi ya watoto kati ya umri wa miaka 19-28 ambao wanajiita mdomo wa furu, mbio za vijiti, Jamaica mokaz,wanaume nenge, west lawama, wanaovamia raia wema kwa kuwakata na nyembe, kuchoma visu na kufanya uvamizi katika majumba. Aidha amewatoa hofu wananchi wa Mji wa Musoma kuhusu taarifa isiyo sahihi ya mauaji ya watu 17 ya kukatwa vichwa, na kwamba katika matukio hayo hakuna mauaji ya watu hao bali ni uvamizi wa kawaida na kwamba tukio la mauaji ya mtu kukatwa kichwa lipo lakini si idadi iliyotajwa na ni kwa Wilaya ya Butiama.

No comments:

Post a Comment