MUSOMA VIJIJINI (MAJITA)
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Musoma limegawanyika kwa mara ya kwanza na kufanya baadhi ya madiwani kutoka nje na kususia kikao baada ya kutofatiana kimtazamo juu ya ugawaji wa halmashauri ndani ya wilaya ya Butiama.
Tofauti
hiyo ilitokea Agosti 7 wakati wa kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo ambayo makao makuu yake
bado yapo ndani ya Manispaa ya Musoma.
Baadhi ya madiwani hasa upande wa kambi
ya upinzani walikuwa wakidai kuwa wananchi wa kata ambazo zimegawanywa
na kuwa halmashauri ya Musoma hawatatendewa haki endapo watakuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Butiama.
Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Bukima Ruti Mayamba alisema
wawo kama wawakilishi wa wananchi hawatakuwa wamewatendea haki kutoka
kata za majita na Lukuba kwani watakuwa mbali na huduma za kiutawala .
Mayamba alisema huduma zitakuwa karibu endapo watakuwa chini ya mkuu wa wilaya ya Manispaa ya Musoma.
“Tunataka kata hizi kumi na saba ziungane na kata 13 za Manispaa ya Muasoma ili kutengeneza wilaya ya Musoma”,alisema Mayamba.
Kwa upande wa madiwani wa
chama Tawala waliazimia kuwepo na halmashauri mbili ya Musoma na
Butiama ndani ya wilaya ya Butiama ambazo zitakuwa chini ya Mkuu wa
wilaya hiyo ya Butiama.
Kikao cha baraza la
madiwani ndicho kikao kilichotajiwa kutoa maamuzi ya mugawanyo huo wa
hamashauri mbili zilizopo ndani ya wilaya ya Butiama ambapomapendekezo
yalielekezwa kuwepo na halmashauri mbili za musoma na Butiama ambazo
zitakuwa chini ya Mkuu wa wilaya ya Butiama kwa kupigwa kura.
Katika mgawanyo huo wa halmashauri mbili zenye jumla ya kata 34, katika halmashauri
ya Musoma kuna 17 ambazo ni pamoja na Nyegina,Etaro,Nyakatende,Mugango,
Kiriba ,Bukumi,SugutiNyamrandirira,Nyambono,Bugwema,
Murangi,Bukima,Buringa,Bwasi,Makojo,Tegeruka na Busambara ambapo makao
makuu ya halmashauri hiyo yatakuwa Suguti-Kwikonero.
Halmashauri
ya Butiama nayo inakata 17 ambazo ni Nyankanga,Buruma,Bukabwa,Bwiregi,Nyamimange,Buswahili,Sirolisimba,Mirwa,Buhemba,Muriaza,Kukirango,Busegwe,Butiama,Masaba,Bisumwa
na Kyanyari ambapo makao makuu ya halmashauri hiyo yatakuwa Butiama
No comments:
Post a Comment