TAASISI ya Kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa
Mara, imemfikisha Mahakamani Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ,Christopher
Nyandiga kwa makosa ya kutumia nyaraka zenye lengo la kumdanganya mwajiri wake
kinyume cha sheria na kuisababishia serikali hasara ya jumla ya Sh Milioni 24.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
kusainiwa na Naibu Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa, Yustina Chagaka imesema kuwa
Mhandisi huyo ambaye kwa sasa yuko Wilaya ya Ledewa alifanya makosa na
kudanganya mwajiri wake kinyume na kifungu cha 22 cha sheria ya kuzuia na kupambana
an rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 na kifungu cha 10(1) cha jedwali la wkanza
kikisomwa pamoja na vigungu vya 57(1) na 60(2) vya sheria ya uhujumu uchuni Namba
200 kama ilivyofanyiwa mapitio mwaka 2002.
Ilisema baada ya uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU umebaini kuwa kampuni inayomilikiwa na
mshitakiwa iitwayo Mbully Enterprises and Covil Works ilipewa zabuni na
halmashaur ya Wilaya ya Bunda ya kutoa Wind mill aina ya Poldaw ya mita
5.8/mita 8.2 kwa gharama ya Sh. Milioni 24, kuisimika (installation) kwa gharama ya Sh. Milioni 2, kuifanyia majaribio (testing) kwa gharama ya
Sh. Milioni 1 na Jumla yake ikiwa Sh Milioni 27 kwa ajili ya mradi wa
umwagiliaji mazao katika kijiji cha Kasuguti.
Aidha uchuguzi uliofanywa umebaini kuwa Mnano Disemba 2007
kwa niaba ya Kampuni hiyo iliyowasilisha hati ya madai(invoice) namba 0152 na
delivery note namba 0252 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda zenye
maelekezo ya uongo.
Maelezo hayo yalisema kuwa alinunua na kuwasilisha Wind Mill
moja aina ya Poldaw ya mita 8.2 yenye thamani Sh Milioni 24 huku akijua kuwa si
kweli kwa sababu Wind Mill hiyo haikuwa ya Poldaw ya Mita 8.2 bali ilikuwa
chakavu ambayo haifai kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa Mkoa wa Mara inatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutoa
ushirikiano kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa.
No comments:
Post a Comment