Wednesday, August 8, 2012


MUSOMA.

Madiwani wa Manispaa ya Musoma wametakiwa kusimamia
ukusanyaji wa mapato kikamilifu ili kuiwezesha Manispaa kupata fedha
zitakazotumika kuwahudumia wananchi wake.

Hayo yamesemwa na Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika jana katika ukumbi wa Manispaa.

Alisema halmashauri hiyo ya manispaa inavyo vyanzo vingi vyamapato,ambavyo vikikusanywa  vizuri vitasaidia katika kuboresha huduma muhimu kwa wananchi kama vile huduma ya maji na barabara..

Naye Mchumi wa Manispaa ya Musoma John Masero alisema baadhi ya Madiwani na watumishi wa Manispaa wanatuhumiwa kwa kuwa na maslahi binafsi katika suala la kutoa zabuni mbalimbali katika Manispaa.

Masero alilieza baraza hilo kuwa  hayo kufuatia baadhi ya Madiwani katika baraza hilo kushinikiza kupunguzwa kwa masharti katika mchakato wa kutoa zabuni hali ambayo  itaipunguzuia Manispaa mapato.

Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Kigera Charles Ocharo ameziomba Idara husika
kufanya uchunguzi juu ya  tuhuma hizo ili wote watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria.

Manispaa inatajia kujenga barabara za Mitaa kwa kiwango cha Lami na katika Mitaa kadhaa sanjali na kuweka vibao vya Mitaa ya baadhi ya  majina ya  waasisi wake ili waendelee kuezniwa ikiwa pamoja na Mtaa wa  Lucas Musiba eneo la Nyasho Kona, ambao kibao chake hakijulikanai kilipelekwa wapi.

No comments:

Post a Comment