Saturday, August 18, 2012

MAKARANI WA SENSA WAENDA FIELD

 MUSOMA.

MAKARANI wa Sensa, katika Sensa ya watu na Makazi Wilaya ya Musoma Mjini wanaendelea na Mafunzo ya vitendo ambapo wamekwenda kutembelea maeneo ya kazi (AE) watakazofanyia kazi kwa kuzitambua.

Katika zoezi hilo ambalo liligawanyika kwa makundi makundi kwa makarani wa Dodoso fupi walikwenda maeneo mbalimbali wakiongozwa na Ramani zilizopo.

Aidha wamekwenda maeneo ya Kitaji B,C,D Mwigobero na Iringo ambapo wamebaini Mambo mbalimbali na baadae mchana huu watafanya majumuisho kwa wakufunzi wa Madarasa.

Semina hiyo itamalizika kesho ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kufunga mafunzo hayo na Makarani hao kuanza kazi ifikapo usiku wa Tarehe 25/8/2012 usiku wa manane.

Wakati huo huo zoezi la kuandikisha vitambuliho vya makazi liko Mbioni ambapo ianelezwa kwamba linatajiwa kuanza mara baada ya zoezi la Sensa ya watu na makzi kuisha.

Mafunzo kwa makarani wa Sensa yalianza wiki iliyopita na kufunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome.



 

No comments:

Post a Comment