MUSOMA
MBIO za Mwenge wa Uhuru zinaanza Agosti 13 katika Mkoa wa Mara ambapo utawasili
katika Kijiji cha Robanda Wilaya ya Serengeti na kupokelewa Nabi -Gate ambapo kutafanyika makabidhiano kati ya Mkoa wa
Arusha na kuingia Mkoa wa Mara.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Mara, inasema Mara baada ya kuokelewa utaanza mbio zake kwa kuzindua miradi
mbalimbali ya Maendeleo.
Miradi itayowekewa jiwe la Msingi ni pamoja na Sekondari ya
Robanda, kisima cha Motukeri, jengo la kituo cha wakulima Natta na kupokea
taarifa ya ujenzi.
Ukiwa Wilaya ya Serengeti Mwenge huo utafanya uzinduzi wa nyumba bota ya
mwanakijiji wa Nyichoka,kupokea taarifa ya mwenye nyumba nay a ujenzi wa jengo
la huduma ya Mama na Mtoto na kufungua jengo pia kuweka jiwe la msingi katika
ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ambapo zawadi na cheti zitatolewa kwa club ya wapinga
rushwa.
Aidha katika Wilaya ya Tarime Mwenge huo utafungua SACCOS ya
Masanga,kuweka jiwe la Msingi kituo cha Afya cha Nyanungu, kutembelea shamba la
Migomba la ekari tanio na kuzindua uvunaji maji ya mvua matenki mawili,
kufungua jengo la utawala la Magoto Sekondari, kufungua ofisi ya Kata ya
Nyarero,kuzindua daraja la Ronsoti na barabara yenye urefu wa Mita800, wodi ya
Wazazi ya hospitali ya Wilaya,mradi wa kitalu cha kahawa na chai.
Mwenge huo ukiwa katika Wilaya hiyo pia utazindua klabu ya
kuzuia rushwa na madawa ya kulevya, kufungua zahanati ya Ikoma, kuzindua kisima
cha maji katika Sekondari ya Mirare, kufungua Saccos na kuweka jiwe la msingi
Utegi Saccos, utatembelea hifadhi ya mazingira na ufugaji wa nyuki pamoja na
kukabidhi Mizinga mitano ya nyuki na kisima cha Maji na kuweka jiwe la msingi
baabara ya Buturi sekondari na kufanya ukaguzi wa Kilimo cha umwagiliaji na
kukabidhi power tiller nne,Trekta mbili na mashine ya kukoboa mpunga na
kutembelea kikundi hc kuteketeza nyavu haramu kilichoko Kinesi.
Katika Manispaa ya Musoma Mwenge huo utaweka jiwe la misngi
kwenye nyumba bora ya mwananchi, kufungua mradi wa maji Shule ya Sekondari ya
Ufundi,kuweka jiwe la msingi maabara ya sekondari ya Bweri na kuzindua klabu ya TAKUKURU, kuweka jiwe la
msingi katika wodi ya watoto iliyoko Nyakato, kuweka jiwe la msingi ujenzi wa
barabara ya Kwangwa kilometa 2, kufungua vyumba vinne vya madarasa shule ya
msingi kigera na kupanda miti ya vivuli na matunda pia kufungua Kantini ya Chuo cha VETA.
Utafungua pia jengo la kuhifadhi maiti(Mochwari), kukagua na
kuhasisha kikundi cha vijana cha useremala na Saccos ya akinamama iliyoko uwanja wa Mpira wa Karume na kutoa hundi ya Sh. 100,000.
Agosti 17 Mwenge huo utaelekea katika Wilaya ya Butiama
ambapo makabididhiano yatafanyika kijiji cha Nyankanga na kuelekea Butuguri.
No comments:
Post a Comment