Monday, July 11, 2011

WAZIRI NAHONDA AWAKA MARA.

SERIKALI imesema kuwa uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara uliopo Nyamongo wilaya ya Tarime umeandaa mkakati wa kuandaa maaskari wao ili kutatua migogoro ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kuwa inasababishwa na maaskari polisi mgodini hapo.

Akizungumza katika kikao na waandishi wa habari katika ukumbi wa uwekezaji wa Mkoa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha baada ya kumaliza ziara yake ya kutathmini ulinzi na usalama mkoani hapa .

Alisema baada ya kuzungumza na wazee wa jadi wanaouzunguka mgodi huo,kamati ya uongozi wa menejimenti ya mgodi huo na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa serikali imegiza uongozi wa mgodi kuandaa maaskari wao kutatua matatizo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara .

“Mei 5 mwaka huu kulitokea vurugu kubwa katika mgodi wa Nyamongo ambapo watu kadhaa walipoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa ambapo sharia yetu hairuhusu mtu yeyote kutolewa uhai pasipo sababu zozote”Alisema Nahodha.

Alisema ili kumhenzi Mwasisi wa Taifa hili Hayati Mwalimu Julius Nyerere ambaye alikuwa mzaliwa wa hapa, Mkoa wa Mara hauna budi kufanya hivyo kwa kuwa alisisitiza kuendeleza amani na alikuwa msitari wa mbele kutatua migogoro mingi ya kiafrika, hivyo itakuwa aibu kubwa sehemu aliyozaliwa Mwalimu kuwa na migogoro.

Alisema kuwa Mgodi huo ndio mgodi pekee ambao unazungukwa na wananchi ambapo ni hatari sana, hivyo Mkoa umeazimia kila mwananchi aliyepo eneo hilo atoe gharama zake mali zake zote alizonazo ili aweze kulipwa pesa na kupisha shuguli za mgodi kuendelea.

“Tumeona kuwa utatuzi mwingine wa wananchi waliopo katika eneo linalozunguka mgodi ni pamoja na kuhama eneo hilo,sasa wao wakae, na nimemwagiza Waziri anayehusika aje na ashugulikie suala hilo kwa amani ili wananchi wetu waliendelee kunyanyasika na jambo la nyongeza ya hapo,ili kuhakikisha wananchi wanakuwa katika hali ya usalama,tunezungumza na uongozi wa mgodi kuweka uzio wa ukuta katika sehemu hiyo na ama kutenga sehemu ya wachimbaji wadogo wadogo” Alisisitiza Nahodha.

Dola M.10 zimetegwa kwa ajili ya kusafisha maji ambayo yatasaidia wanachi waliopo katika vijiji hivyo na kwamba uongozi wa mgodi umehaidi kununua mtambo wa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo na kwamba uongozi huo tayari umetenga dola 100,000 kwa kila kijiji kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo watachagua wenyewe.

Vijiji hivyo ni Nyankunguru, Nyamwaga, Matongo, Nyangoto, Kerende, Kewanja, na Genkuru.

Akikemea maaskari wanahusika na mauaji ya makusudi katika eneo hilo alisema serikali haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria na kuwataka kutumia kazi yao kwa busara ya hali ya juu kwani bila kufanya hivyo askari hataipenda kazi yake, na kwamba askari anapokuwa katika mazingira magumu inamlazimu kupambana na ndio maana inalazimika kuwepo na mauaji, pia wananchi wanahitaji kupewa elimu ili waweze kuelewa.

Akizungumzia hali ya umaskini iliyopo katika vijiji saba vinavyozunguka mgodi huo alisema kuwa kumekuwepo na makubaliano baina ya uongozi wa mgodi na wenyeviti wa vijiji ambayo yalipagwa na hayakutekelezwa.

Alisema kwa kuwa mpango huo wa kuwalipa fidia haukutekelezwa serikali imeandaa mkataba na kwamba utangaliwa kwa pande zote kuanzia serikali ya Mkoa, Uongozi wa mgodi, wananchi wenyewe na halmashauri yenyewe ambao utazingatia matakwa ya wananchi.

Kuhusu vitambulisho vya uraia alisema Sh. B.355 zimetegwa kwa ajili ya kutengengeza vitambulisho ambapo tayari mkandarasi kutoka nchi ya Malasia ameweka mkataba na serikali kwa ajili ya kuanza kazi hiyo na ameahaidi kuwa mwishoni mwa mwaka huu atakuwa ameishatoa vitambulisho vya awali ambapo vitaanza vitambulisho vya wafanyakazi kwa awamu ya kwanza,wanafunzi awamu ya pili na wafanyabiashara awamu ya tatu.

Alisema uamuzi wa kuanza na wafanyakazi utazingatiwa kwani utaondoa usumbufu katika malipo kwani baadhi yao ulipwa fedha wakati wameishafariki.Waziri anaendelea na ziara Mkoa wa Kagera Wilaya ya Ngara.