Friday, April 13, 2012

MIAKA 10 YA MFUKO WA BIMA YA AFYA

WADAU wa Bima ya afya wameilamikia kamati za afya za kata kuwa hazifanyi kazi ipasavyo kwa kuwa hazitoi taarifa za wanachama wa Bima kutokana na kukosekana kwa madawa kwa wanachama wake.

Akizungumza katika Mkutano wa wadau wa masuala ya Bima ya afya na kusherekea miaka 10 ya mfuko wa afya ya jamii (CHF) tangu uanzishwe, Mkurugenzi wa tiba Mafao na Ushauri(DMTS), Dk. Frank Lekey aliwataka madiwani wa kata kuhakikisha wanafuatilia na kutoa taarifa kuhusiana na dawa zinazoletwa kwa wanachama zinawafikia walegwa.

Aliwataka watanzania kubadilika na kuacha kasumba ya kuchangia misiba badala ya kuchangia huduma ya afya kwa mgojwa katika mfuko wake, ili aweze kupata huduma ipasavyo kuliko mgojwa kupoteza maisha jambao ambalo linapoteza nguvu kazi ya Taifa.

Akitoa Mada katika Mkutano huo Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Mara, Dk. Leonard Mitti alisema kuwa changamoto zinazoukabili Mfuko huo ni pamoja na kusimama kwa michango ya baadhi ya wanachama, baadhi ya halmashauri kushindwa kuwasilisha michango ya asilimia 3 ya Madiwani kwenye mfuko huo kwa mujibu wa sheria, wanachama waliokoma utumishi kutorejesha vitambulisho na idadi ndogo ya kaya zinazojiunhga na CHF na kutumia vitambulisho vya wizi.

Alisema kuwa hadi kufikia Disemba 2011 Mkoa wa Mara ulikusanya michango ya wanachama kiasi cha Sh. M. 36,811,948.

Naye Mwanasheria wa Mfuko wa afya ya jamii (CHF), Christina Ilumba akitoa mada alisema changamoto za CHF ni pamoja na ufinyu wa wanachama, upungufu wa dawa katika ituo vya tiba, kujitoa kwa wafadhili wanaolipia makundi maalum, matumizi Masaya ya fedha za Mfuko yasiyojali ununuzi wa madawa na baadhi ya watendaji kutotoa huduma stahiki kwa wanachama wa mfuko.

Aliongeza kuwa waratibu wa CHF wanaoteuliwa na Halmashauri wawe ni wale wanaofanya kazi za maendeleo ya jamii kama mafisa maendeleo ya jamii na kwa Halmashauri ambazo Mratibu wa NHIF na CHF ni mmoja inapaswa waongeze mtu mwingine mmoja ili kuongeza ufanisi.

Akitoa ushauri kwa wanachama Bima ya afya wasikatishwe tamaa na huduma zinazotolewa na wauguzi hasa katika hospitali za Serikali kwa kutochagia pesa taslimu na kupeleka na kadi pekee, kwani wao ndio wanaolipa pesa nyingi kuliko watu wengine wowote.

Akifungua Mkutano huo kwa naiba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara,John Tuppa, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isaack alisema ni vyema mfuko huo usiwe na ubaguzi wowote kutokana na kutofautisha kadi kulingana na viwango vya Mishahara kwani vinaleta unyanyapaa unaosababisha kutopata huduma za iliyo nzuri na ya haraka.

“Watu wote wapewe huduma sawa bila kuangalia kipato cha mtu, ni vizuri mfuko huu ukawa na kadi moja ili kuondoa matabaka ya walionacho na

wasionacho ili huduma ziwe sawa kwani ugojwa hauna kadi” Alisema Isaack.

Alisema kuwa Ni ukweli ulio wazi kuwa gharama za matibabu zinapanda kila uchao, hivyo njia pekee ya kumkomboa Mtanzania ni kumpa uhakika wa kutibiwa yeye na familia yake kupitia mfumo wa Mfuko wa Afya ya Jamii ambao NHIF uko chini yao.

“Nawaomba fanyeni kazi zenu kwa moyo mmoja mkijua kuwa mafanikio ya CHF ni ndoto ya kila kiongozi katika ngazi zote za serikali. Tumieni wakati wenu kuelimisha wananchi kuwa, raslimali ndogo walizo nazo za mifugo au mazao wanayozalisha zinaweza kuboresha afya zao kwani hakuna uzalishaji bila uwepo wa Afya bora” Alisema Tuppa.

Alisema Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo wananchi wake wanachangamkia sana fursa za maendeleo kila zinapojitokeza. Lakini kwa bahati mbaya haijaonyesha mwamko wowote katika kuchangamkia fursa ya utaratibu rahisi wa kuchangia matibabu kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

“ Takwimu zinaonyesha kuwa hadi mwezi Disemba mwaka jana, kati ya kaya 237,071 zilizopo katika mkoa wa Mara , ni kaya 1,460 tu ya kaya zilizojiunga na CHF hiyo ni sawa na asilimia 0.6 ya kaya zote, tunajiuliza tatizo ni nini? Ni kweli wananchi wa Mkoa wa Mara hawana uwezo wa kuchangia Shilingi 10,000 kwa kaya kwa mwaka” Aliuliza Mkuu huyo wa Mkoa.