MUSOMA.
WAZIRI wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa, amewataka
wananchi wa Mkoa wa Mara, kutunza Mkongo wa Taifa kwani una manufaa makubwa kwa
uchumi wa Taifa hili.
Ilikuwa ni siku ya kukamilisha ziara yake ya siku moj akatika Mkoa wa Mara,Wilayani Tarime mji wa Sirari mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa
Mkongo huo na changamoto zinazoukabili.
Alisema
Mkongo wa Taifa una manufaa makubwa kwa uchumi wa Taifa hili kwa kuwapatia mawasiliano wananchi wake, ambapo Mikoa ya
Tanga na Arusha ina watumiaji wengi na Mkoa wa Mara bado haujawa na watumiaji wengi,
ambapo pia kuna changamoto mbalimbali zinazoukabili ikiwa ni pamoja na maporoko
upande wa Arusha ambapo udongo umekuwa
ukiingia kwenye miundo mbinu ya Mkongo huo.
Aliwahadharisha
wananchi kuwa nyaya za Mkongo huo zina madhara makubwa kwa kuwa zimetengezwa
kwa kioo maalumu, hivyo unaweza kuharibu Mkongo huo, huku ukiambulia upofu,
kwani nyaya zake ni hatari sana ziiingiapo kwenye jicho.
“Ni kosa
kubwa kuhujumu miundo mbinu, wananchi waelewe kuwa miundo mbinu hii ni kwa
ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla,pia hakuna shaba katika mkongo huu, ambayo wahujumu wanafikiri kuwa ipo, ila nyaya zake
ni nyuzi laini kama unywele ambapo waya
huo ni hatari sana kwani unaweze kukutia upofu” Alisema Mbarawa.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Kammpuni ya Simu ya
Tanzania ( TTCL), Mkoa wa Mara na Posta, katika ofisi zake zilizopo mkabala na
uwanja wa Michezo wa Karume, alisema kuwa wafanyazi hao wana thamana kubwa ya kuutunza kwani ndio waliokabidhiwa jukumu hilo.
“TTCL yaani
nyie mmepewa jukumu la kuuendeleza mkongo kwa maana ya kuusambaza nchi nzima
kwa niaba ya Serikali ili kuleta ubora wa huduma kwa gharama nafuu, usalama wa
nchi, watu na mali zao” Alisema Mbarawa.
Alisema kuwa
Serikali inataka kufanya ubia kati ya Bat
Airtel ya India na TTCL ambapo Bat Airtel yuko tayari kuachia hisa zote kwa
Kampuni ya TTCL na kwamba kwa sasa kila kampuni iko kwenye mchakato wa
kutathimini hisa zake na kwamba tayari Bat Airtel wamekamilisha.
Kwa upande
wa Shirika la Posta nchini aliwataka wafanyakazi kuwa wabunufu kwani
teknolojia zinabadilika na kwamba Wizara itaaendelea kushirikina na Shirika hilo hili liweze kukua kwani
lisiposaidiwea linaweza kupotea.
Alizitaka
taasisi zote za Serikali kutumia huduma ya
shirika hili kwa kutuma vifurushi vyote kwa njia ya posta kwani kuna
baadhi ya Taasisi za Serikali zimeacha kutumia Shirika hilo, na hivyo kusababisha
kukosa mapato.
Kuhusu
nyongeza ya Mishahara ambayo watumishi wa Posta walimlilia Waziri aliwataka kutuma
maombi yao kwa bodi, ambayo ndiyo yenye thamana ya kufikia maombi yao hazina na
hazina ikashughulikia hivyo ana imani kuwa nyonyeza ya mshahara inawezekana
kwani Serikali yao ni sikivu.