Tuesday, January 7, 2014
TAARIFA ZA KIPOLISI MKOA WA MARA
JESHI la polisi Mkoa wa Mara linawashikilia watu wawili kwa kupatikana na madawa ya kulevya aina ya mirungi katika kijiji cha Kirumi Wilaya ya Butiama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara (SACP) Ferdinand Mtui amesema kuwa tukio hilo lilitokea Jan 3 katika kizuizi cha Kirumi ambapo askari walifanikiwa kuwakamata Mseti Fedrick (20) na Sando Wakuru (18) wote wakazi wa Tarime wakiwa wa kilo 100 za madawa ya kulevya aina ya mirungi wakitumia pikipiki yenye namba za usajili T.697 BNV SUNLG.
Wakati huo huo mtu mmoja amefariki dunia kwa kuliwa na mamba wakati anavua samaki mto Lubana,ulioko maeneo ya Tamau kata ya Kuzugu Tarafa ya Serengeti Wilaya ya Bunda.
Amesema tukio hilo lilitokea mnamo Januari 4 mwaka huu ambapo amemtaja kuwa ni Mashaka Lazaro (48) na mkazi wa kijiji cha Ligamba.
Katika tukio jingine Mnamo Januari 6 majira ya saa 5:30 eneo la Mkirira kata ya Nyegina, Tarafa ya Makongoro Wilaya ya Butiama Mkoani hapa, mwendesha pikipiki Akuku Aringo(47) mkazi wa Nyakato Mlimani katika Manispaa ya Musoma aliuawa kwa kukatwa katwa na mapanga kichwani, mikono yote na kuvunjwa miguu yote kisha kuchomwa moto na wanachi akidaiwa kuiba mihogo katika shamba ambalo mmiliki wake hajajulikana.
Kamanda anaendelea kuwasisitiza wananchi kutojichukuliwa sheria mkononi ba kutoa taarifa za wahalifu kwenye vyombo vya dola ili sheria ifuate mkondo wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)