TARIME.
Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Mara, kupitia Mwenyekiti wake, Christopher Sanya amesema Chama hakina imani na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewelle,kwani amekuwa akikejeri viongozi wa kitaifa wa CCM na kwamba hawana maamuzi yoyote bali yeye ndiye mwenye maamuzi.
"kuna kila sababu ya msingi ya kumkataa Mkuu huyu kutokana na kauli zake za kejeri ambazo amekuwa akizitoa mbele ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Tarime" Alisema Sanya.
Aidha wamemuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua za haraka za kumuondoa Mkuu huyo ndani ya siku 21 na kuwaletea Mkuu mwingine ili kusaidia uchaguzi wa Serikali za Mitaa waweze kupata ushindi ndani ya Wilaya hiyo.
Ikumbukwe kuwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tuppa,alipoteza maisha akiwa katika ofisi ya Mkuu huyo wa Wilaya ambapo alitokwa povu mdomoni, cha kushangaza, katika ziara ya Balozi wa China, Dk. Lu Youqing alisaini kitabu cha wageni katika hotel ya Gold Land iliyoko Tarime badala ya ofisini.