MUSOMA.
Kampuni Mama ya TTCL imelalamikiwa kutofanya kazi vyema kutokana na mtandao wake kusuasua, na kusababisha kutofanyika vyema kwa mafunzo ya waandishi wa habari za mtandao katika zama za Internet yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika MISA TAN,katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi( VETA),Mwisenge Mkoa wa Mara, yanayoendelea.
Waandishi wa habari wamepata wasiwasi mkubwa kutoka na mafunzo yanayoendelea kwa wanafunzi wa Chuo hicho kama wanafundisha vyema,kutokana na kukatikatika kwa mtandao Chuoni hapo.
Maafisa wa TTCL, waliotafutwa kujibu ni kwa nini kuna tatizo hilo, hawakupatikana na mmoja wao,aliyejulikana kwa jina moja la Mlimila simu yake ilikuwa haipatikani.
Wakufunzi katika mafunzo hayo ni Mhariri wa Luninga ya Star TV,Flora Rugashoborola na Mwakilishi wa MISA TAN,Sengiyumva Gasirigwa