Wednesday, March 9, 2016
MTANZANIA WA KWANZA KUMILIKI MGODI
MJUE mtanzania wa Kwanza na Wilaya ya Kwanza Tanzania kumiliki mgodi wa Dhahabu, si mwingine ni Nyakilang'ani Mauza Mkazi wa Musoma Manispaa, aliyewatoa aibu wafanyabiashara wengi ambao hawana wazo la kuwa na biashara ya kuchimba madini nchini Tanzania licha ya kuwa rasilimali za madini zipo nchini na huwa tunawaachia wawezekezaji kutoka nchi kuja kuwekeza na kuondoka na mali nyingi nchini kwentu bila kuacha faidi yoyote nchini kwetu.
Mauza amejenga Mgodi katika Halmashauri ya Musoma Vijijini,Wilaya ya Butiama kijiji cha Kataryo, ambapo ameshirikiana na nchi ya Canada, mgodi huo unaitwa CATA MINING kwa maana ya Ushirikiano wa TANZANIA NA CANADA.
zaidi ya Bilioni 108 zimetumika katika ujenzi wa Mgodi huo ambapo kati ya hizo Dolla Milioni 34 ni mkopo kutoka Benki ya CRDB na Dolla Milioni 20 ni kutoka Benki ya TIB na zilizosalia ni kutokana na jitihada zake.
Wakati Mgodi huu uko mbioni kuanza kazi, mkandarasi wa umeme Sengerema Engineering Group hajafikisha umeme huo,licha ya kupewa kazi ya ujenzi wa njia ya umeme yenye ukubwa wa KV33 na alilipwa fedha asilimia 50 ya kazi Julai, 2014 lakini kazi aliyoifanya haijafikia nusu ya kazi yake.
lakini hapa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhogo anatoa amri kwa Mkandarasi huyo kuhakikisha anapeleka umeme haraka vinginevyo atafutwa kwenye orodha ya wakandarasi.
“Ni uzembe wa hali juu sana, mpaka sasa mgodi huu hauna umeme, kama atashindwa atafutwa kwenye mradi wa REA, yuko wapi..aje hapa kesho ndege zipo anieleze kwa nini mpaka sasa hakuna umeme hapa, watu wa Tanesco mko wapi, hamjui kuwa mgodi huu ukianza kazi ni fedha kiasi gani zitaingia katika Shirika? Harakikisheni Mzalendo huyu apate Umeme”.Alisema Muhongo huku akiwa amekunja uso.
Meneja wa Mgodi huo, Peter Bourhill anasema kuwa Mgodi huo unatarajia kutoka kilogramu 30-50 kwa mwezi ambapo mwezi Mei na Juni mwaka huu vifaa vya uzalishaji kutoka Canada vitaanza kuingia ili Mgodi uanze uzalishaji.
Subscribe to:
Posts (Atom)