Wednesday, December 6, 2017
MBUNGE MATHAYO ATOA MILIONI 1.7 ZA KUONGEZA MITAJI KWA WAFANYABIASHARA.
MUSOMA.
WAKAZI wa kata ya Nyamatare wamemwomba Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo kuhakikisha anawaletea maji katika soko la biashara la Nyamatare kwani wanatumia maji ya dimbwi la maji machafu yaliyochimbwa kwa ajili ya ujenzi wa Choo katika soko hilo.
Wameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara wa kutambulisha viongozi wapya wa Wilaya hiyo waliochaguliwa katika chaguzi zilizopita wiki iliyopita.
Mkazi wa kata hiyo, Christina Mori ambaye ni mfanyabiashara katika soko hilo alisema kuwa kutokana na huduma duni ya maji iliyopo wanalazimika kuchota maji kwenye dimbwi la maji machafu kwa matumizi ya kuosha viazi vitamu ambavyo kwa kawaida huwa na udongo kutokana na kutokuwa na maji hali mbayo inahatarisha afya ya wananchi hao.
Changamoto zilizopo katika soko na kata hiyo kwa ujumla ni pamoja na huduma ya choo,uvujaji wa maji ovyo kutokana na ujenzi wa miundo mbinu ya barabara na mitaro.
Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma, Magiri Maregesi ametoa wiki mbili kwa mamlaka ya maji safi na taka Manispaa ya Musoma, (MUWASA) ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa ukakika kwani ulazaji wa mabomba ya maji umeishamalizika na uko mita kadhaa kuelekea katika soko hilo.
Naye Diwani wa kata hiyo, Masumbuko Magesa aliilalamikia Mamlaka hiyo kwa uzembe uliofanyika wa kutowasiliana kati ya mamlaka zote,na kusababisha mabomba ya maji kuwa ya ya mitaro ahali ambayo inahatarisha usalama wa mabomba ambayo yanaweza kuhujumiwa na ahata kuharibika.
Kwa upande wa vivuko vya barabara, Diwani huyo alilalamikia ucheleweshaji wa ujenzi wa vivuko ambao inawalazimu wananchi kupata hadha kubwa wakati wa matatizo yanapotokea hasa kwa upande wa huduma ya maziko ama panapotokea mgonjwa hali ambayo inawaletea hadha kubwa wananchi wa eneo hilo.
Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Fidelica Muyovella alisema kuwa barabara ya Nyasho-Nyamatare-Majita inahitaji jumla ya vivuko 65 lakini vitajengwa vivuko 20.
Katika kuongeza mitaji kwa wanawake wajasiliamali, Mbunge huyo alitoa kiasi cha Sh. Milioni 1.7 akishirikiana na viongozi wapya waliochaguliwa ili kuinua uchumi wa mwanamke na kuahidi kuwajengea mabanda mengine,ikiwemo uzio na choo.
Subscribe to:
Posts (Atom)