Sunday, June 10, 2018

WAZIRI LUKUVI AKIANGALIA MPAKA WA KENYA.



Mtaalamu wa upimaji, Huruma Lugalla akimwonyesha Waziri wa Ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi moja ya alama zilizopo katika mpaka wa Tanzania na Kenya Wilaya ya Rorya kijiji cha Kilongwe Mkoa wa Mara, kushoto kwa mtaamu huyo ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adamu Kigoma Malima na aliyevaa kofia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Doroth Mwanyika.

Tuesday, May 29, 2018

IJUE TFDA



TFDA herufi zake zimetafsiriwa kwa lugha ya kiingireza ikiwa na maana ya Tanzania Food and Drugs Authority, ikiwa na maana kuwa Mamlaka ya Chakula na dawa Tanzania.


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yenye jukumu la kudhibiti ubora na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi


TFDA imepewa madaraka ya kufanya maamuzi mbalimbali ya kiutendaji kwa mujibu wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 na ile ya Wakala za Serikali, Sura 245
Mamlaka ilianza kutekeleza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai, 2003

Dira ya TFDA ni kuwa Mamlaka inayoongoza barani Afrika katika kudhibiti usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi kwa wote
Dhima ya Mamlaka ni kulinda afya ya jamii kwa kuzuia madhara ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na matumizi ya chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi

Majukumu ya TFDA

Kutathmini na kusajili vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi
Kudhibiti utengenezaji, uingizaji na usambazaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba na vitendanishi
Kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa viwanda vya utengenezaji na maeneo ya mauzo ya bidhaa zinazodhibitiwa ili kuhakikisha viwango vilivyowekwa vinafikiwa


Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kuhakikisha kuwa bidhaa husika zinafikia viwango vya ubora na usalama
Kusimamia majaribio ya dawa mpya na vifaa tiba
Kutoa leseni na vibali mbalimbali vya kuendeshea biashara ya vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba

Kudhibiti utoaji wa matangazo ya biashara ya bidhaa zinazodhibitiwa na TFDA
Kuratibu madhara yatokanayo na utumiaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Kuelimisha jamii kuhusu ubora, usalama na matumizi sahihi ya bidhaa zinazodhibitiwa

Mamlaka ina ofisi saba (7) za Kanda ambazo ni kaskazini, Arusha, Manyara, Tanga, na Kilimanjaro, kanda ya ziwa, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mwanza na Kagera, kanda ya mashariki, Pwani na Dar es Salaam,kanda ya kati, Dodoma, Morogoro na Singida,Kanda ya juu Kusini Mbeya Iringa, Njombe Songwe na Rukwa , kanda ya Kusini, Mtwara, Lindi na Ruvuma, kanda ya Magharibi ni Tabora, Kigoma na Katavi.
Muundo.


Mamlaka pia inashirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa katika kuhakikisha kuwa sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 inatakelezwa ipasavyo
Baadhi ya madaraka na majukumu ya TFDA yamekasimiwa kwa Halmashauri chini ya Kifungu Na. 121 cha Sheria na kupitia Kanuni za Kukasimu Madaraka na Majukumu ya TFDA kwa Halmashauri (GN No. 476) za mwaka 2015 na marekebisho yake GN No. 19 ya mwaka 2017

Wadau wa Mamlaka
Wizara na Idara mbalimbali za serikali
Mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi mbalimbali
Mashirika ya kimataifa (WHO, FAO, UNICEF)
Watengenezaji, waingizaji nchini, wasambazaji na wauzaji wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Vyombo vya Habari (Wahariri/Waandishi)
Wasimazi mbalimbali wa sheria
Wafanyakazi wa sekta ya Afya na watafiti
Vyama vya wafanyabiashara wa bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka ikiwa ni pamoja na wajasiriliamali
Watoa huduma mbalimbali
Walaji, watumiaji na wananchi wote kwa ujumla


Mafanikio

Kuwa na mifumo ya usajili, ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara wa bidhaa
Kufikia kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 katika utendaji bora wa kazi
Maabara ya dawa ya TFDA kutambuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)
Maabara ya Chakula na Mikrobiolojia ya TFDA kupata ithibati (Accreditation) kwa kiwango cha kimataifa cha ISO/IEC 17025:2005
Kusogeza huduma karibu na jamii kwa kufungua ofisi saba (7) za Kanda na kuajiri wakaguzi katika vituo vya forodha Kuboresha ufanisi katika utoaji huduma kwa kutumia mifumo ya TEHAMA
maombi mbalimbali kufanyiwa kazi kwa njia ya mtandao (online system)
Kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa kutoa taarifa za madhara yatokanayo na
dawa (ADR reporting system) Mifumo mingine –LIMS, HR-MIS

Changamoto zinazoikabili Mamlaka
Jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu majukumu ya TFDA na hivyo kutokutoa mchango wa kutosha katika kuhakikisha kuwa sheria inatekelezwa
Kutokuwepo kwa mifumo iliyowianishwa ya udhibiti wa bidhaa kati ya Tanzania na nchi za jirani (EAC, SADC, n.k)

Mabadiliko ya haraka ya teknologia, utandawazi na soko huria unaosababisha ongezeko la bidhaa katika soko hivyo kuongeza ugumu wa udhibiti
Kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wadau wasiofuata masharti ya sheria kwa hiari


Friday, May 18, 2018

Ajali Mbaya yatokea Musoma.


Ajali ilitokea Mei 13 katika eneo la Nyasho, baina ya gari aina ya scania namba T299 BXR likiwa na kibeba mizigo namba T858 BTB, lililokuwa linaendeshwa na Masha Mstapha ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo,ambapo aligonga gari aina ya Nadia Namba T248 BSG ambapo Didi Msira Koko na mkewe, Joyce waliumia vibaya na kukatika miguu ambapo wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza.dreva wa bajaji ya harusi, Baraka Suguti hali yake pia siyo nzuri, yeye anaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya Musoma, anasema hana uwezo angeenda Mwanza, scania hilo liliingia kwenye duka spea za magari la Mang'ombe Joseph.

Sunday, January 28, 2018

WAZIRI MKUU NA UWANJA WA NDEGE MUSOMA


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, juu ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Musoma katika uwanja wa ndege wa Musoma ambayo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mara. Kiwanja hicho kitajengwa hivi karibuni, uwanja huu ukimalizika utaongoza pato la Mkoa wa Mara na Manispaa ya Musoma.

Wednesday, December 6, 2017

MBUNGE MATHAYO ATOA MILIONI 1.7 ZA KUONGEZA MITAJI KWA WAFANYABIASHARA.



MUSOMA.

WAKAZI wa kata ya Nyamatare wamemwomba Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, Vedastus Mathayo kuhakikisha anawaletea maji katika soko la biashara la Nyamatare kwani wanatumia maji ya dimbwi la maji machafu yaliyochimbwa kwa ajili ya ujenzi wa Choo katika soko hilo.

Wameyasema hayo katika Mkutano wa hadhara wa kutambulisha viongozi wapya wa Wilaya hiyo waliochaguliwa katika chaguzi zilizopita wiki iliyopita.

Mkazi wa kata hiyo, Christina Mori ambaye ni mfanyabiashara katika soko hilo alisema kuwa kutokana na huduma duni ya maji iliyopo wanalazimika kuchota maji kwenye dimbwi la maji machafu kwa matumizi ya kuosha viazi vitamu ambavyo kwa kawaida huwa na udongo kutokana na kutokuwa na maji hali mbayo inahatarisha afya ya wananchi hao.

Changamoto zilizopo katika soko na kata hiyo kwa ujumla ni pamoja na huduma ya choo,uvujaji wa maji ovyo kutokana na ujenzi wa miundo mbinu ya barabara na mitaro.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Musoma, Magiri Maregesi ametoa wiki mbili kwa mamlaka ya maji safi na taka Manispaa ya Musoma, (MUWASA) ili wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa ukakika kwani ulazaji wa mabomba ya maji umeishamalizika na uko mita kadhaa kuelekea katika soko hilo.
Naye Diwani wa kata hiyo, Masumbuko Magesa aliilalamikia Mamlaka hiyo kwa uzembe uliofanyika wa kutowasiliana kati ya mamlaka zote,na kusababisha mabomba ya maji kuwa ya ya mitaro ahali ambayo inahatarisha usalama wa mabomba ambayo yanaweza kuhujumiwa na ahata kuharibika.

Kwa upande wa vivuko vya barabara, Diwani huyo alilalamikia ucheleweshaji wa ujenzi wa vivuko ambao inawalazimu wananchi kupata hadha kubwa wakati wa matatizo yanapotokea hasa kwa upande wa huduma ya maziko ama panapotokea mgonjwa hali ambayo inawaletea hadha kubwa wananchi wa eneo hilo.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma, Fidelica Muyovella alisema kuwa barabara ya Nyasho-Nyamatare-Majita inahitaji jumla ya vivuko 65 lakini vitajengwa vivuko 20.
Katika kuongeza mitaji kwa wanawake wajasiliamali, Mbunge huyo alitoa kiasi cha Sh. Milioni 1.7 akishirikiana na viongozi wapya waliochaguliwa ili kuinua uchumi wa mwanamke na kuahidi kuwajengea mabanda mengine,ikiwemo uzio na choo.

Thursday, November 30, 2017

MJUE MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA MARA (Musoma Mjini)


Mmiliki wa Blog hii akiingia katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Mara, amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Mara kutoka Wilaya ya Musoma, na alishinda kwa kishindo katika nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa, ikiwa ni Wilaya moja ya Musoma, ikiwa imeungana na Musoma Vijijini ambayo ni Wilaya kichama kwa sasa.

WAGOMBEA WAKIJINADI.


Wegesa Hassan Witimu akipiga magoti kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Mkoa wa Mara, kuomba ridhaa ya kuwa Mwenyekiti,katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa CCM, Mkoa wa Mara, Wilaya ya Musoma Mjini.