WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Utatibu wa Bunge pia Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Mh. William Lukuvi amewaasa wale wote wenye tabia za kukikumbatia Chama Cha Mapinduzi CCM kuwa ni Chama kutoka mifukoni mwao waache tabia hiyo mara moja ili kurudisha heshima na Chama na wananchi kukiamini Chama chao.
Aliyasema hayo juzi katika kilele cha Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama ambapo kimetimiza miaka 35 sasa tangu kuzaliwa kwake, Wilaya ya Serengeti Mugumu mara alipokamilisha matembezi ya msikamano kukumbuka kuzaliwa kwa Chama.
Waziri huyo aliongoza matembezi ya mshikamano kutoka katika ofisi za Chama hicho mpaka viwanja vya mbuzi na kuhudhuriwa na baadhi ya wanachama wakiwemo viongozi wa Chama Mkoa na Wilaya, Wakuu wa Wilaya wa Wilaya za Musoma na Serengeti akiwemo Mkuu wa Mkoa.
Maadhimisho hayo yaliyotarajiwa kufanyika kimkoa katika Wilaya ya Serengeti, yaliadhimishwa kwa kila Wilaya ambapo kila Wilaya zilifanya matembezi yao ya mshikamano kujikumbushia Chama kilipotoka, kiko wapi na kinakwenda wapi.
Alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama wamekifanya Chama Cha Mpianduzi kuwa Chama kutoka mifukoni kwao na kutozingatia maamuzi na ushauri kutoka kwa viongozi wengine.
Akizunguza katika Ukumbi wa Mikutano wa Musoma Mjini alipokutana na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Mkoa na Wilaya, Makatibu kata, Madiwani na wajumbe wa kamati za utekelezaji wa Wilaya za Musoma Vijijini na Mjini aliwaasa kuacha tabia hiyo ili kukiweka Chama pazuri.
Aliwataka kujiimarisha wao wenyewe kwanza,kabla ya kuimarisha Mikoa mingine, ukizingatia kuwa Mkoa huo ni bigwa wa kupigia kampeni Mikoa mingine huku wao wakiwa nyuma.
“Nyinyi mnasifika kwa kupanga siasa za Mikoa ya wenzenu Mkoa wa Mara mko wachache sana lakini mkiamua jambo likuwa la kweli! Kweli! Mbona kwenu mnashinda. Mnasifika sana kwa kupanga siasa za mikoa mingine, Irekebisheni ya kwenu kabla ya kurekebisha ya wenzenu” Alisema Lukuvi huku ukimya ukitawala katika Ukumbi huo.
Aliwaasa kutumia uwezo huo walionao kujipanga upya na kuhakikisha Chama kinashinda kuanzia ngazi ya Shina na Matawi unaotajia kuanza mwezi huu.
“Safari hii hakikisheni mnachagua viongozi bora watakaoweza kukiongoza Chama na wenye moyo wa kujituma na uwezo wa kuwashawishi wanachama ili kupata ushindi, na wajue kuwa watakuwa na kibarua kigumu” Alisisitiza Lukuvi.
Alitumia fursa hiyo kumtaka kila mwana CCM, kutoka maoni yao juu ya mabadiliko ya katiba Mpya pindi tume itakapokuja kukusanya maoni.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Utaribu wa Bunge na Mlezi wa Mkoa wa Chama Mkoa alizindua Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambalo hadi kukamika kwake limegharimu kiasi cha Sh. M. 26.
Awali kabla ya uzinduzi huo aliwataka wananchi kutumia kwa uangalifu chakula walichopata na kuacha tabia ya kuuza mazao nje ya nchi na baadae kuiomba serikali kuleta chakula cha msaada, huku akizitaja wilaya za Bunda, Musoma Vijijini na Musoma Mjini kuwa waombaji wa misaada.
Kuhusu fedha zinazoletwa kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali aliwataka madiwani wafuatilia kama fedha hizo zinatumika ipasavyo kwani kuna baadhi ya miradi haitekelezeki na matokeo yake wananchi wanaichukia serikali yake kwa baadhi ya watu wachache walio na ubadhilifu wa fedha. Wilaya hiyo imepewa B.19.7
Waziri pia alizindua Shina la kikundi cha Wajasiamali wadogo wa CCM wanaojishughulisha na fani za ufundi Seremala, Vyuma, cherehani, Uashi, Ususi na Upakaji rangi (SECHUWARA) wa Wilaya ya Serengeti ambapo alijibu risala yao kwa kuendesha mchango wa papo kwa papo ambapo Sh. M. 1.5 zilipatikana, ambazo zitawasaidia kuendeleza biashara ambapo pia aliagiza Halmashari kuwatafutia eneo ambalo watafanya shughuli zao bila kulipia ili kupunguza gharama na kuhakikisha kikundi hicho kinapata usajili ili waweze kupata mikopo.