Musoma
CHAMA cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Mkoa wa Mara wameonesha
kusikitishwa na Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani
wanaosimamia na kuhakikisha matumizi bora na sahihi ya barabara
wamegeuka kuwa hakimu wa makosa yote, pia wamepinga adhabu kwa mtu
aliyehukumiwa kuua kwa kukusudia ahukumiwe kifo na kusema kuwa hiyo
sio sahihi na wala haki.
Kauli hiyo ilitolewa na Wakili Baraka Makowe kwa niaba ya chama hicho
ambapo alisema kuwa askari hao wa barabarani wamekuwa wakitoza faini
kwa kwa mamlaka ambayo wamepewa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya
OCD na si Kamanda wa usalama barabarani (OCS) ama kamanda wa usalama
barabarani Mkoa (RTO).
“ kanuni za utoaji adhabu hazifuatwi wakati sheria
inaelekeza vipi atendewe mkosaji wa mara ya kwanza, mkosaji mzoefu na
kwa kiwango gani cha adhabu kitolewe, wenzetu leo kila kosa hutoza
faini ya shilingi 30,000,”alisema Wakili Makowe.
Alisema kuwa maudhui ya siku ya sheria nchini yanayohusu faida za
adhabu mbadala kwa jamii, hazitakosewa wakiendelea kusisitiza kuwa
adhabu huambatana na hatia na shurti itamkwe na kutolewa na na taasisi
yenye mamlaka hayo kisheria.
“Si kwa sera, mazoea au matakwa, kufanya hivyo ni kosa na ni kinyume
cha sheria, nataka kwanza tujikite katika utoaji wa adhabu mbadala
ndipo tuangalie faida husika. Kwa kuwa jambo hili ni pana, juhudi za
kulichambua kwa undani zitafanyika na hivyo huenda ikaathiri mtiririko wa uwasilishaji wa mada lakini nina imani tutagusa sehemu zote muhimu,”alisema.
Alisema kuwa kutokana na kupitia maudhui ya Adhabu mbadala katika kesi
za jinai, na faida zake kwa jamii kwa niaba ya chama cha mawakili wa
Tanganyika muda muafaka umefika na vifungu vya 197 na 26 (1) vya sura
ya 16 ya sheria za nchi vitazamwe upya.
“Ni muda muafaka kwa adhabu mbadala itumike na iamriwe hadi kugusa
kesi za mauaji ya kukusudia, pia kwamba hata vile vifungu vya 195 (1)
na 198 vya sheria hiyo navyo vitazamwe upya. Kwamba si jambo jema mtu
akae gerezani hadi atakapokufa adhabu mbadala yaweza kutolewa kwake,”
alisema.
Naye Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mkoa huo, Hussein Mushi alisema
kuwa adhabu mbadala inafaida nyingi katika jamii ambapo baadhi ya
faida ni pamoja na kupunguza msongamano magerezani ili kuipunguzia
serikali gharama za kuendesha magereza kwa kupunguza watu wanaotegemea
huduma magerezani.
“Hii ni pamoja na kuishirikisha jamii kwa kuwarekebisha wahalifu na
kuwawezesha wahalifu kuendelea kutunza na familia zao huku wakiendelea
kutumikia vifungo vyao, kutoa mchango wa maendeleo kwa jamii pale
wafungwa wa kifungo cha nje wanaposhiriki katika ujenzi wa wa shule,
hospitali, barabara, utunzaji wa mazingira na usafi katika ofisi za
umma hali itakayoipunguzia serikali gharama za shughuli hizo, alisema
Mushi.
Pia alitoa onyo kwa wananchi kuacha tabia ya kuingilia shughuli za
huduma za jamii wajue kuwa ni kinyume cha sheria na ni kosa la jinai
na mtu anapotiwa hatiani atapaswa kulipa faini ya shilingi Laki 5 au
kifungo cha miaka miwili jela au vyote viwili.
siku ya sheria nchini na inahashiria mwanzo wa shughuli za mahakama kwa mwaka 2012 ambapo maudhui yake ni adhabu mbadala katika kesi za jinai, faida zake katika jamii ambapo hufanyika mwezi wa pili wa kila mwaka.
No comments:
Post a Comment