KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Nape Nnauye amekabidhi mifuko 400 ya simenti kwa Mkoa wa Mara kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa ambayo ni pungufu.
Akikabidhi mifuko hiyo kwa Katibu huyo, Mfanyabiashara ambaye ni Mkazi wa Mkoa wa Mara, Zulfikar Nanji,alisema amehamasika kusaidia jamii ya Mkoa huo kutokana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa akipokuwa akizungumzia upungufu wa madarasa uliopo katika Mkoa huo ambao umesababisha baadhi ya wanafunzi kutoendelea ma shule.
“Nimehamasika kutokana na kusikia kwenye vyombo vya habari taarifa ya Mkuu wa Mkoa akizungumzia juu ya upungufu wa madarasa yaliyosababisha baadhi ya watoto kukosa nafasi za kuendelea na masomo yao, nikaona si vyema na mimi kama mzaliwa wa Mkoa huu sina budi kuisaidia” Alisema Nanji.
Akitoa shukrani kwa mfanyabiashara huyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye alisema wakati Chama kinaelekea kutimiza miaka 35 ya kuzaliwa kwake bado kiko imara na kitaziki kuwa imara kutokana na kwamba kinatekeleza ilani ya CCM.
“Wakati tukielekea katika maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM, tunapata matukio mengi mazuri na yanayoashiria kukuwa na kuendelea kwa Chama kilichosheheni ubora, Amani na Utulivu wa nchi yetu” Alisema Nnauye.
Wakati wa makabidhinao hayo aliyofanyika katika uwanja wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, wakereketwa na viongozi wa CCM, pia walijitokeza kuunga mkono msaada huo, akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, MNEC, Vedastus Mathayo akiyehaidi mifuko 100 ya simenti, Diwani wa kata ya Nzela Wilaya ya Geita Mkoa wa Mwanza, Joseph Msukuma ambaye pia akiahaidi mifuko 100, na Diwani Mstaafu wa kata ya Bweri Wilaya ya Musoma Mjini, Isaack Chacha ambaye pia aliahidi mifuko 20 ya simenti.
Akizungumzia upungufu wa madarasa uliopo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa alisema jumla ya madarasa 239 yanatakiwa kujengwa ili watoto wapatao 6,486 ambao mpaka sasa wako majumbani kufikia mwezi Machi wawe wameanza shule.
Wilaya zenye uhaba mkubwa ni Wilaya ya Bunda ambayo ina upungufu wa madarasa 88, Musoma vijijini madarasa 46 na Musoma Mjini madarasa 26
No comments:
Post a Comment