Friday, June 15, 2012

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA


JUMLA ya wahamiaji haramu na walowezi  wapatao 319 wamekamatwa kwa kipindi cha Januari- Mei Mwaka huu.

Akizungumza na BLOG hii ofisini kwake, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mara, Jacob Sambai alisema kuwa kati ya hao wapo waliofikishwa mahamakani na wapo walirurejeshwa kwao pia waliotumikia kifungo.

Alisema kuwa kati ya hao wapo Wakenya 259, Wathiopia 44, Warundi nane,Wasomali watatu, Waganda watatu na Wakongo wawili.

Alisema kuwa  hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuwafukuza nchini ambapo waliofukuzwa ni wapatao 197 kutoka nchi mbalimbalimbali na wanaoendelea kuchunguzwa ni 39, waliokutwa ni wakimbizi ni nane, waliofugwa kwa amri ya mahakama ni tisa na kwa wale ambao kesi zao ziko mahakamani ni saba, waliogundulika ni watanzania kutoka na mwingiliano na kufanana kwa lugha kati ya makabila ya Wakurya wa Kenya na Wajaluo wa Kenya ni tisa na walioharalisha ukazi ni 60.  

Alisema kuwa Idara hiyo ina changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na uhalifu wanaofanyiwa wafanyakazi wawapo kazini kuchomwa visu hadharani,Mauaji,  uvamizi wa kutumia silaha hali ambayo inahatarisha maisha yao, ubora na ufanisi wa kazi jambo ambalo watumishi wamekuwa na hofu kubwa ya kufanya kazi huku wakihofia usalama wao.

“Kuna baadhi ya wenzetu si vizuri kuwataja majina yao waliwahi kuvamiwa kwa kutumia silaha,kwa bahati njema walipona na wengine kuchomwa visu wakiwa kazini,madhalani basi limekuja na abiria unawaambia washuke ili wagongewe hati ya kusafiria passport, ghafla anakuja mtu usiyemfahamu anakutaka vidole, mmoja wetu alifanyiwa hivyo, sasa hii ni hatari sana” Alisema Sambai.

Alisema kuwa chagamoto zingine zinazoikabili Idara hiyo ni pamoja na  mwingiliano wa makabila kati ya Wakenya wa kabila la Wajaluo na Wakenya wa kabila la Wakurya ambao wanafanana tabia na  Wakurya Watanzania na Wajaluo wa Tanzania, kwa hiyo inakuwa ngumu kuwatofautisha na kuwatambua kutokana na lugha zao kufanana na baadhi yao wamekuwa na mahusiano ya kindugu, Uhaba watumishi na ukosefu wa nyumba za watumishi.

Aidha kumekuwepo na baadhi ya viongozi wakiwemo wenyeviti wa vijiji na baadhi viongozi wa vyama vya siasa hasa madiwani wamekuwa na asili ya wakenya, hivyo inakuwa ngumu kumtaja mtu ambaye ameingia nchini na anaishi bila kibali kutokana na mahusiano kati yao jambo ambalo limekuwa likikwamisha utendaji kazi.

Ukubwa wa mipaka umekuwa changamoto kubwa kwa idara hiyo kutokana na urefu wake na umbali kwa vituo vya ukaguzi vya Kogaja na Shirati kuwa nje ya mpaka, hivyo ni vyema zikahamishwa ili kuweka ufanisi wa kazi na kufufuliwa  kwa kituo cha Bolega kilichoko Wilaya ya Tarime ambapo awali kilikuwa na msaada mkubwa.

.

Alisema kuwa kwa mwaka huu Idara ya Uhamiaji Mkoa huu imeweza kutoa semina katika Tarafa zipatazo nane zenye kata 56 na vijiji au mitaa 210 katika Wilaya za Bunda Tarafa ya Kikopya na Chamriho, Wilaya ya Rorya Tarafa ya Girango  na Tarafa ya Nyancha, Wilaya ya Serengeti Tarafa ya Logolo na Gurument, Wilaya ya Tarime Tarafa ya Nyancha,vijiji vya Ichange na Inchugu, Wilaya ya Musoma inatarajiwa kufanyika katika Tarafa ya Nyancha na Makongoro.

Semina hizo zilikuwa na  lengo la kuweka ufanisi na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ambapo namba za simu za viongozi zilitolewa kwao ili kutoa taarifa panapotokea mtu ameingia nchini na anaishi bila kuwa na vibali pia aliwasisitiza viongozi hao kuwapa moyo wananchi kwani wamekuwa na uwoga wa kuwataja wahamiaji haramu kutokana na kuhofia usalama wao wa kuhatarisha maisha.


Friday, June 1, 2012

MADINI TUNAYO BARABARA HAIPITIKI NYAMONGO





TARIME.

ABIRIA na Madereva wanaofanya safari zao kupitia barabara ya Nyamwaga kuelekea Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara  Wameitaka  Serikali kukarabati barabara kwa viwango vinavyotakiwa kwa  madai kuwa barabara itokayo Nyamwaga hadi Nyamongo imedaiwa kuwa kero kutokana na miundombinu mibovu ya barabara.

Walisema kuwa kuendelea kuwepo kwa ubovu wa barabara na kutokarabatiwa inawapa kero nakwamba wakati mwingine hulazimika  kushuka toka ndani ya gari na kutembea kwa miguu pindi magari yakwamapo.

Wakiongea na  mwandishi wa mwananchi juzi ambaye naye alikuwa miongoni kati ya wasafiri waliokuwa wanakwenda Nyamongo na kisha kukwama  eneo la Kumarera-Nyamwaga kutokana na ubovu wa barabara walisema kuwa wanapata hasara na usumbufu pindi  magari yakwamapo ambapo huwalazimu kuchukuwa usafiri wa pikipiki huku wasiokuwa na pesa wakitembea kwa miguu kutoka maeneo mabovu ya barabara hadi mahali waendako kwa mwendo wa zaidi ya kilomita 10.

“Abiria tunapata kero na usumbufu kutokana na ubovu wa barabara ukifika eneo la Nyamwaga hadi Nyamongo barabara ni mbovu magari yanakwama  inabidi watu washuke kutafuta utaratibu mwingine wa usafiri kama pikipiki ulipe pesa nyingine na wakati huo uchukuwe na usafiri mwingine kwa ajili ya kubeba mizigo yetu inatupa hasara sisi wasafiri”alisema Bhoke Chacha mkazi wa kijiji cha Nyangoto- Nyamomgongo.

Abiria hao walisema kuwa kukwama kwa magari  kunasababisha wasifike kwa wakati unaotakiwa mahali waendako kutokana na magari hayo kuchukuwa muda mrefu safarini na kwamba kwa wale waendao vijiji vya mbali hulazimika kulala katika nyumba za wageni( Guest) Nyamongo huku wengine kuhairisha kuendelea na safari na kurudi watokako.

“Barabara  ikarabatiwe kwa kiwango kinachotakiwa,kwa kawaida kutoka mjini Tarime hadi Nyamongo kwa usafiri wa gari ni dakika 45 lakini kutokana na ubovu ni zaidi ya saa moja na nusu,nauli toka Tarime hadi Nyamongo ni 5,000 gari linapokwama  inabidi ulipe tena 5,000 kwa ajili ya usafiri wa pikipiki  na kama una mzigo unalipia pikipiki nyingine 5,000 unajikuta unatumia zaidi ya 15,000, Serikali isipuuze irekebishe barabara, na kuna siku magari yalikwama  eneo la kumarera yakaondoka usiku wa saa 3 na eneo hilo ni hatari kwa usalama, watu utekwa na kuporwa vitu na wengine walishajeruhiwa eneo hilo”alisema Nicolaus Coronelio Mtendaji wa kata ya Matongo-Nyamongo.

Mmoja kati ya Madereva wa magari anayefanya safari zake kutoka Tarime hadi Nyamongo alisema kuwa kuendelea kuwepo kwa ubovu wa barabara hiyo imekuwa ni kero baina yao na abiria ambapo pia alisema huingia gharama kubwa za mafuta kutokana na kutumia muda mrefu kusafiri njiani.

“Ubovu wa barabara unatupa kero madereva barabara ina mashimo mengi  mvua ikinyesha magari yanakwama,yakikwama inabidi tuwarudishie abiria nauli ukikataa kurudisha nauli ni mgogoro tunaingia hasara kutokana na umbali mlefu tunaokuwa tumetoka magari yakikwama abiria wanaondoka zao tunabaki sisi madereva na magari yetu inatubidi twende kwenye miji kuomba majembe walau kurekebisha kidogo ”alisema Bunini.

 Aliongeza” maeneo mengi ya barabara ni mabovu akija kiongozi wa kitaifa barabara inatengenezwa kwa haraka usiku na mchana inaripuliwa wiki mbili zikipita inarudi katika hali yake ya ubovu kama kawaida ukarabati unaofanyika kwenye barabara siyo ule wa viwango vinavyotakiwa inalipuliwa”alisema Dereva Chacha Bunini mkazi wa Nyamongo.

Kuendelea kuwepo kwa ubovu wa miundombinu ya barabara  wasafiri wamekuwa wakipata shida hasa wakati wa mvua ambapo mnamo Mei 25 zaidi ya Magari 50 yalikwama katika eneo la Kumarera-Nyamwaga kwa muda wa zaidi ya sa 6 baada ya magari hayo yaliyokuwa yakifanya safari zake kati ya Tarime,Nyamongo na Mugumu kukwama na hivyo kuladhimu abiria kushuka na kutafuta usafiri wa pikipikina wengine kutembea kwa miguu.

Mhandisi Mkuu wa barabara(Tanroad) Mkoa wa Mara Emanuel Koroso alipoelezwa  malalamiko ya ubovu wa barabara pamoja na kumtaka kutoa taarifa za gharama zilizotengwa na zilizotumika  kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa barabara ya Nyamwaga alisema barabara hiyo   haimuhusu yeye bali  mhusika wa barabara hiyo ni Mgodi wa North Mara Barrick ambaye Mkansarasi wake ni Kampuni ya Casco inayofanyashughuli zake ndani ya mgodi wa North Mara.

Uongozi wa Mgodi wa dhahabu wa North Mara Barrick kupitia Afisa habari Robert,,,,,,,,, walipotakiwa kujibu  malalamiko ya wananchi kuhusu Ukarabati wa barabara unaofanywa na mgodi huo hawakuwa tayari kusema lolote.

Mkuu wa Wilayani John Henjewele alipoulizwa msimamizi  wa barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwa wasafiri kutokana na ubovu wa barabara alisema kuwa barabara ya Nyamwaga hadi Mugumu iko chini ya Tanroads ambapo alihimiza kuwa wakandarasi wanaoajiriwa na mgodi wanapaswa kufuata vigezo sawa na wale wanaokodiwa na Serikali na inapojengwa au kukarabatiwa kwa viwango vinavyotakiwa  mkandarasi anatakiwa awajibiswhe mara moja.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,