TARIME.
ABIRIA na Madereva wanaofanya
safari zao kupitia barabara ya Nyamwaga kuelekea Nyamongo Wilayani Tarime
Mkoani Mara Wameitaka Serikali kukarabati barabara kwa viwango vinavyotakiwa
kwa madai kuwa barabara itokayo Nyamwaga
hadi Nyamongo imedaiwa kuwa kero kutokana na miundombinu mibovu ya barabara.
Walisema kuwa kuendelea
kuwepo kwa ubovu wa barabara na kutokarabatiwa inawapa kero nakwamba wakati
mwingine hulazimika kushuka toka ndani
ya gari na kutembea kwa miguu pindi magari yakwamapo.
Wakiongea na mwandishi wa mwananchi juzi ambaye naye
alikuwa miongoni kati ya wasafiri waliokuwa wanakwenda Nyamongo na kisha
kukwama eneo la Kumarera-Nyamwaga
kutokana na ubovu wa barabara walisema kuwa wanapata hasara na usumbufu
pindi magari yakwamapo ambapo huwalazimu
kuchukuwa usafiri wa pikipiki huku wasiokuwa na pesa wakitembea kwa miguu
kutoka maeneo mabovu ya barabara hadi mahali waendako kwa mwendo wa zaidi ya
kilomita 10.
“Abiria tunapata kero na
usumbufu kutokana na ubovu wa barabara ukifika eneo la Nyamwaga hadi Nyamongo
barabara ni mbovu magari yanakwama
inabidi watu washuke kutafuta utaratibu mwingine wa usafiri kama
pikipiki ulipe pesa nyingine na wakati huo uchukuwe na usafiri mwingine kwa
ajili ya kubeba mizigo yetu inatupa hasara sisi wasafiri”alisema Bhoke Chacha
mkazi wa kijiji cha Nyangoto- Nyamomgongo.
Abiria hao walisema kuwa
kukwama kwa magari kunasababisha
wasifike kwa wakati unaotakiwa mahali waendako kutokana na magari hayo
kuchukuwa muda mrefu safarini na kwamba kwa wale waendao vijiji vya mbali
hulazimika kulala katika nyumba za wageni( Guest) Nyamongo huku wengine kuhairisha
kuendelea na safari na kurudi watokako.
“Barabara ikarabatiwe kwa kiwango kinachotakiwa,kwa
kawaida kutoka mjini Tarime hadi Nyamongo kwa usafiri wa gari ni dakika 45
lakini kutokana na ubovu ni zaidi ya saa moja na nusu,nauli toka Tarime hadi Nyamongo
ni 5,000 gari linapokwama inabidi ulipe
tena 5,000 kwa ajili ya usafiri wa pikipiki
na kama una mzigo unalipia pikipiki nyingine 5,000 unajikuta unatumia
zaidi ya 15,000, Serikali isipuuze irekebishe barabara, na kuna siku magari
yalikwama eneo la kumarera yakaondoka
usiku wa saa 3 na eneo hilo ni hatari kwa usalama, watu utekwa na kuporwa vitu
na wengine walishajeruhiwa eneo hilo”alisema Nicolaus Coronelio Mtendaji wa
kata ya Matongo-Nyamongo.
Mmoja kati ya Madereva wa
magari anayefanya safari zake kutoka Tarime hadi Nyamongo alisema kuwa
kuendelea kuwepo kwa ubovu wa barabara hiyo imekuwa ni kero baina yao na abiria ambapo pia
alisema huingia gharama kubwa za mafuta kutokana na kutumia muda mrefu kusafiri
njiani.
“Ubovu wa barabara unatupa
kero madereva barabara ina mashimo mengi
mvua ikinyesha magari yanakwama,yakikwama inabidi tuwarudishie abiria
nauli ukikataa kurudisha nauli ni mgogoro tunaingia hasara kutokana na umbali
mlefu tunaokuwa tumetoka magari yakikwama abiria wanaondoka zao tunabaki sisi
madereva na magari yetu inatubidi twende kwenye miji kuomba majembe walau
kurekebisha kidogo ”alisema Bunini.
Aliongeza” maeneo mengi ya barabara ni mabovu
akija kiongozi wa kitaifa barabara inatengenezwa kwa haraka usiku na mchana
inaripuliwa wiki mbili zikipita inarudi katika hali yake ya ubovu kama kawaida ukarabati unaofanyika kwenye barabara siyo
ule wa viwango vinavyotakiwa inalipuliwa”alisema Dereva Chacha Bunini mkazi wa
Nyamongo.
Kuendelea kuwepo kwa ubovu wa
miundombinu ya barabara wasafiri
wamekuwa wakipata shida hasa wakati wa mvua ambapo mnamo Mei 25 zaidi ya Magari
50 yalikwama katika eneo la Kumarera-Nyamwaga kwa muda wa zaidi ya sa 6 baada
ya magari hayo yaliyokuwa yakifanya safari zake kati ya Tarime,Nyamongo na
Mugumu kukwama na hivyo kuladhimu abiria kushuka na kutafuta usafiri wa
pikipikina wengine kutembea kwa miguu.
Mhandisi Mkuu wa
barabara(Tanroad) Mkoa wa Mara Emanuel Koroso alipoelezwa malalamiko ya ubovu wa barabara pamoja na
kumtaka kutoa taarifa za gharama zilizotengwa na zilizotumika kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa
barabara ya Nyamwaga alisema barabara hiyo haimuhusu yeye bali mhusika wa barabara hiyo ni Mgodi wa North
Mara Barrick ambaye Mkansarasi wake ni Kampuni ya Casco inayofanyashughuli zake
ndani ya mgodi wa North Mara.
Uongozi wa Mgodi wa dhahabu
wa North Mara Barrick kupitia Afisa habari Robert,,,,,,,,, walipotakiwa
kujibu malalamiko ya wananchi kuhusu
Ukarabati wa barabara unaofanywa na mgodi huo hawakuwa tayari kusema lolote.
Mkuu wa Wilayani John
Henjewele alipoulizwa msimamizi wa
barabara hiyo ambayo imekuwa kero kwa wasafiri kutokana na ubovu wa barabara
alisema kuwa barabara ya Nyamwaga hadi Mugumu iko chini ya Tanroads ambapo
alihimiza kuwa wakandarasi wanaoajiriwa na mgodi wanapaswa kufuata vigezo sawa
na wale wanaokodiwa na Serikali na inapojengwa au kukarabatiwa kwa viwango
vinavyotakiwa mkandarasi anatakiwa
awajibiswhe mara moja.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
No comments:
Post a Comment