KATIBU wa CCM Wilaya ya Butiama,Mkoa wa Mara, Mercy Mollel
amewatahadharisha wagombea katika nafasi mbalimbali ili kujiepusha na rushwa pindi
wanapoomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari
ofisi kwake na kutangaza majina ya wagombea katika nafasi mbalimbali ndani ya
Chama.
Alisema wakereketwa wengi wamejitokeza katika kuomba nafasi
mbalimbali za uongozi kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chenye mvuto
kwa jamii kubwa kutokana na sera zake zinazoaminika na kwamba ndhicho
kinachoongoza nchi.
Alisema katika nafasi ya Ujumbe Mkutano Mkuu wa CCM Taifa
waliojitokeza ni wanachama wapatao 43,ambapo
katika mchujo wanachama wapatao 15 ndio walioteuliwa ambapo watatakiwa wajumbe
watano, aliwataja kuwa ni Nyageti Adamu, Eva-Sweet Musiba,Bhoke Ngurube,
Rosemary Orinda, Wegesa Witimu,Vivian Juma,Joseph Magere, Brasius Chuma,
Fidelis Kisuka, Gerald Kasonyi, Sebastian Makakira, Rashid Gewa, Jerome Masawe,
Nyabukika Nyabukika, Magige Nyerere.
Aidha katika nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi walijitokeza wanachama wapatao tisa,
ambapo waloiteuliwa kugombea nafasi hiyo ni wajumbe wapatao watatu nao ni, Bwire
Gibuma Ntobi Zedesi Ntobi na Japhet Werema,nafasi ya Uchumi na fedha waliojitokeza
walikuwa sita na waliopita katika mchujo ni Baraka Imanyi (Obama), Haruni
Munema na Magina Nyauko.
Katika nafasi ya Ujumbe Mkutano CCM Mkoa waliojitokeza ni
Wegesa Witimu,Break Chisumo, Yohana Munema, Rudia Mazera, Nestory Matiko na
Happiness Nyamasagara.
Alisema kuwa katika kundi la wanawake jumla ya wakereketwa
wapatao 32 walijitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, walioteuliwa ni
Thabita Idd, Wegesa Witimu, Mwajuma Magoti na Bhoke Ngurube,ambapo Wazazi
walioteuliwa kugombea ni Fidelis Kisuka, Wambura Kishemuri, Ihunyo Marwa, John
Nyamisana, Ibrahim Makanya na James Matongo.
Alisema kuwa kwa upande wa kundi la vijana nafasi ya Ujumbe
wa Halmashauri Kuu ya Wilaya walijitokeza wagombea wenye umri mkubwa na hivyo
kusababisha kutoteuliwa.
Aliongeza kuwa kwa upande wa nafasi za Mwenyekiti na Wajumbe
wa NEC yanasubiriwa kutoka Halmashauri Kuu Taifa irejeshe majina ya wanachama walioomba nafasi hizo.