JUMUIYA ZA CCM ZA UWT NA WAZAZI MUSOMA MJINI WAPATA VIONGOZI WAO.
MUSOMA.
JUMUIYA ya Wanawake (UWT) ndani ya Chama Tawala CCM,Mkoa wa Mara imepata viongozi wao
wakaokitumikia Jumuiya kwa Miaka mitano.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hii, ofisini kwake,
Katibu wa UWT Wilaya ya Musoma Mjini Ashura Kimwaga alisema uchaguzi huo
uliofanyika hivi karibuni ulikuwa na Changamoto mbalimbali kwa akina Mama kuwa
na mwamko mkubwa wa kujitokeza kuchukua
fomu za kugombea.
Katika nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo
waliojitokeza kuchukua fomu walikuwa
watano lakini ulipofanyika mchujo watatu waliteuliwa kuchukua,wakiwemo Dinna
Samanyi ambaye alipata kura 111 akifuatiwa na Odina Lujaji ambaye aliambulia
kura saba, huku Amina Masisa akichukua nafasi hiyo kwa kuibuka mshindi kwa
kupata kura 143.
Katika nafasi ya Ujumbe Mkutano Mkuu wa Taifa waliojitokeza walikuwa
wagombea tisa,ambapo nane waliteuliwa katika kinyang’anyiro hicho ambapo nafasi
hiyo inapaswa kuwa na wajumbe watatu,waliopata ushindi ni Godriver Magoti
aliyepata kura 147, Zainabu Musiba(126) na Riziki Hamis(119),naye Rukia Wandwi
ambaye aliwahi kugombea Ubunge viti Maalum akiambulia kura (109), Kura
zilizopigwa zilikuwa 262 na kura moja kuharibika.
Katika nafasi ya Ujumbe Mkutano Mkuu wa Mkoa waliojitokeza
kuchukua fomu walikuwa saba, waliopitishwa walikuwa na nane ambao waliingia
katika mchuano mkali na hatimaye washindi kupatikana,walishinda ni Nyambura
Mtani alipara kura 130 akifuatiwa na Rehema Nyabina alitepata kura 128 na
Twaiba Makangara aliyepata kura 127.
Aidha waliojitokeza katika kuwania nafasi ya Baraza la UWT
walikuwa 12 ambapo waliyeuliwa 11 katika kugombea nafasi hizo, washindi
waliopatikana na kura zao zikiwa kwenye mabano ni Nyambura Kunani(121), Maimuna
Kimaro (108), Naima Minga (98), Rehema Nyambina(95), Stella Mtani (90), Janeth
Mkilimali (88), kura zilizopigwa zilikuwa 262 na kura 10 ziliharibika.
Alisema katika nafasi ya Ujumbe wa halmashauri Kuu ya CCM
Wilaya waliojitokeza walikuwa wawili aliyepata ushindi ni Agness Rambo (122)
huku Maimuna Kimaro akipoteza nafasi hiyo kwa kupata kura 116.
Walipoita bila kupigwa kwa upande wa Mkutano Mkuu wa CCM
Wilaya ni Zainabu Kigera, Wazazi, Riziki Shabani na Vijana ni Lina Lucas.
Akitoa matokeo kwa washindi ndani ya Jumuiya ya Wazazi
Wilaya ya Musoma Mjini, Katibu wa Wazazi Wilaya ya Musoma Mjini, Suzana Sije
alisema nafasi ya Mwenyekiti
ilichukuliwa na Koshuma Koshuma aliyewabwaga wenzake wawili kwa kupata kura
120, na Felix Salumu kura 87 na aliyewahi kuwa Diwani kata ya Kamunyonge
Deogratius Chrispine aliambulia kura 10.
Nafasi ya Ujumbe Halmashauri Kuu na Mkutano CCM, aliyeibuka
mshindi ni Isack Ng’ariba alipata kura 149 huku akiwaacha wenzake kwa mbali
sana akiwemo Sabato Manyasi aliyepata kura 56 na Magreth Wambura kura saba.
Mkutano Mkuu wa Wazazi Mkoa, Juma Meko alishinda kwa kura
161 ambapo Twaiba Mkangara akipata kura 51,nafasi ya Mkutano Mkuu wa Wazazi
Taifa walishinda ni Stella Manyonyi(123), Ally Jama (122) na Masumbuko Magesa
(113),nafasi ya Katibu Elimu, Malezi, Uchumi na Mazingira alipita Phares
Maghubu aliyepata kura 37 akiwatuma wenzake wawili Mayagi Ngeja(11) na Vicent
Malima (4)
Waliopita bila kupigwa katika nafasi ya wajumbe watatu wa Baraza
la Wazazi Wilaya ni Munyu Matara, Jumapili Mbogha na Egdi Manyama.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Butiama, Mercy Mollel alisema
kuwa katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) waliochukua na
kurejesha fomu za kugombea nafasi hiyo ni wagombea wapatao saba akiwemo Mwandishi wa
Habari Eva-Sweet Musiba.
No comments:
Post a Comment