Wednesday, September 19, 2012

MTOTO WA BABA WA TAIFA,MAGIGE NYERERE ULINGONI.

MUSOMA




KATIBU wa CCM Wilaya ya Butiama,Mkoa wa Mara, Mercy Mollel amewatahadharisha wagombea katika nafasi mbalimbali ili kujiepusha na rushwa pindi wanapoomba ridhaa ya kuwatumikia wananchi.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake na kutangaza majina ya wagombea katika nafasi mbalimbali ndani ya Chama.

Alisema wakereketwa wengi wamejitokeza katika kuomba nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho chenye mvuto kwa jamii kubwa kutokana na sera zake zinazoaminika na kwamba ndhicho kinachoongoza nchi.

Alisema katika nafasi ya Ujumbe Mkutano Mkuu wa CCM Taifa waliojitokeza ni wanachama  wapatao 43,ambapo katika mchujo wanachama wapatao 15 ndio walioteuliwa ambapo watatakiwa wajumbe watano, aliwataja kuwa ni Nyageti Adamu, Eva-Sweet Musiba,Bhoke Ngurube, Rosemary Orinda, Wegesa Witimu,Vivian Juma,Joseph Magere, Brasius Chuma, Fidelis Kisuka, Gerald Kasonyi, Sebastian Makakira, Rashid Gewa, Jerome Masawe, Nyabukika Nyabukika, Magige Nyerere.

Aidha katika nafasi ya Katibu wa Siasa na  Uenezi walijitokeza wanachama wapatao tisa, ambapo waloiteuliwa kugombea nafasi hiyo ni wajumbe wapatao watatu nao ni, Bwire Gibuma Ntobi Zedesi Ntobi na Japhet Werema,nafasi ya Uchumi na fedha waliojitokeza walikuwa sita na waliopita katika mchujo ni Baraka Imanyi (Obama), Haruni Munema na Magina Nyauko.

Katika nafasi ya Ujumbe Mkutano CCM Mkoa waliojitokeza ni Wegesa Witimu,Break Chisumo, Yohana Munema, Rudia Mazera, Nestory Matiko na Happiness Nyamasagara.

Alisema kuwa katika kundi la wanawake jumla ya wakereketwa wapatao 32 walijitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo, walioteuliwa ni Thabita Idd, Wegesa Witimu, Mwajuma Magoti na Bhoke Ngurube,ambapo Wazazi walioteuliwa kugombea ni Fidelis Kisuka, Wambura Kishemuri, Ihunyo Marwa, John Nyamisana, Ibrahim Makanya na James Matongo.

Alisema kuwa kwa upande wa kundi la vijana nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya walijitokeza wagombea wenye umri mkubwa na hivyo kusababisha kutoteuliwa.

Aliongeza kuwa kwa upande wa nafasi za Mwenyekiti na Wajumbe wa NEC yanasubiriwa kutoka Halmashauri Kuu Taifa irejeshe majina  ya wanachama walioomba nafasi hizo.




No comments:

Post a Comment