MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Butiama,
Yohana Mirumbe,amesema hataki kuona mpasuko unaotokana na makundi yta Uchaguzi
kwa kuwa kazi hiyo imekwisha na kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii, Umoja
na Mshikamano,
Alisema kuwa wajumbe hao wasimwone kuwa ni kijana na kwamba,
atakayevurunda kazi katika utendaji wa Chama Wilayani humo, atafuata kanuni na
katiba ili kurejesha maadili ya uongozi.
Aliyasema hayo juzi wakati akifungua kikao cha kwanza
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ambacho pia kilifanya tathmin ya uchaguzi na kupendkeza kuwa
wajumbe wawe wanapewa usafiri mzuri kuliko wa awali wa kubeba wajumbe kwenye
malori.
Alisema kuwa atafanya
kazi kwa akushirikiana nao na kwamba viongozia mbao watakuwa wazembe ataanza na
hao.
Kuhusu suala la wagombea wa CCM kunadiwa na vyama vya
upinzani katika nafasi ya NEC, lililoonekana kwa baadhi ya wagombea wa NEC,
Mirumbe alisema si jambo baya kwani wakiwa karibu nao watapata fursa ya
kuwarudisha ndani ya Chama.
“Mimi sioni kama hilo ni tatizo uwenda wakiwa na sisi wanaweza
kuvutiwa na sera zetu na kurejea katika Chama kwani walikuwa huku, kwa upande
wangu ningependa kukaa nao na kubadilishana mawazo, unaweza kupata kitu kipya
kutoka kwao na kuweza kufanya mabadilikoya haraka”Alisema Mirumbe.
Akizungumza na wajumbe hao, Mjumbe wa NEC, Wilaya ya
Butiama, Christopher Siagi, alisema atashirikiana na wajumbe wote katika
kuhakikisha wanapata maendeleo na kuhakikisha suala la usafiri mzuri kwa
kipindi kijachao analivalia njuga.
Naye mgombea wa NEC ambaye kura zake hazikutosha Eva-Sweet
Musiba, alitoa shukrani kwa wajumbe hao na kuwapatia barua za shukrani makatibu
kata kwa kata 34 za Wilaya ya Butiama ikiwa na ujumbe wa kutaka kufanya kazi kwa bidii na
kukumbuka Kilimo ndicho kitakachowakomboa katika maisha yao na kuzingatia elimu
kwa kusomesha watoto wao.
No comments:
Post a Comment