Monday, October 22, 2012

MLEMAVU WA NGOZI AJITOSA NEC VIJANA



DODOMA.

Mlemavu wa  Ngozi Fatma Jumbe Mwalimu amejitokeza kugombea Ujumbe NEC viti 6  na Baraza kuu Taifa viti vitano Bara


Akiwa katika ofisi za Makao Makuu ya Chama Mjini Dodoma alipokuwa akijinadi kwa wapiga kura kutoka Mkoa wa Mara,Mbeya na Kigoma mara walipowasili kutoka Mikoa hiyo 

Alisema kuwa atasimamia maslahi ya vijana kwenye vikao husika,kuipa UVCCM nguvu ya kiuchumi na kimaamuzi na kuimarisha jumuiya na kuhakikisha ushindi wa kishindo ifikapo 2015 katika uchaguzi Mkuu.


Fatma ameongeza kuwa vijana ndiyo nguvu ya Chama na kwamba na kwamba msingi wa maendeleo ya vijana ni vijana wenyewe.

Katika uzoefu ndani ya Chama ni Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM UDSM,Mjumbe Baraza la vijana Mkoa wa Ruvuma, Mjumbe Baraza la UWT Mkoa wa Ruvuma, Katibu Mkuu Jumuiya ya walemavu UDSM (DUAH),Naibu Waziri Maji na Mazingira UDSM, na Afisa afya na mazingira kata ya Ubungo.


Kwa upande wa elimu ana Shahada ya ualimu aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na sasa ni Mwalimu shule ya Sekondari ya wasichana Songea.

Wengine waliokuwa wanajinadi na kutoa vipeperushi vyao ni Beatrice Omolo anayegombea NEC, Nadra Rashid NEC,Edna Kwilasa NEC nafasi 6 Bara,Fadhila Nassor Abdi NEC viti 4 Sango Kasera NEC Zanzibar,Lulu Abdallah NEC viti 4 Zanzibar,Neema Nyangalilo Mgombea NEC,Anthony Mavunde mgombea NEC,Jerry Silaa Mgombea NEC Hassan Chamshama NEC viti sita Bara,Neema Mwandabila NEC nafasi 6 Bara
Esther Sato Makune na Zainabu Katimba wanaogombea Baraza Kuu Taifa nafasi tano,


Wengine niliopata nafasi ya  kuzungumza nao  na kwamba wako imara na kuhakikisha Chama kinaendelea kushika dola ni Mwanawewe Ussi Yahaya anayegombea  BarazaKuu Taifa nafasi tano Zanzibar ,Rashid Gewa  na Asha Abdalla anayegombea Nafasi ya Halmashauri Kuu kupitia UVCCM viti vinne Zanzibar.


Aidha vijana Makao Makuu hapa Dodoma wamepamba Moto zaidi kwa Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Paul Makonda ambapo baadhi ya wajumbe wamekuwa wakibeba bago lako likiwa na maandishi ya heshima, uwezo na utu wa mgombea upimwe kwa mchango wake katika jamii wala sio kundi au fedha alizonazo.

No comments:

Post a Comment