Friday, October 26, 2012

MAJINA YA WALIOMWUA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA YAMETAJWA NA IGP



MWANZA.

NI wiki Moja baada ya ya maziko ya yaliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP ) liberatus Barlow,Jeshi la Polisi limewataja watuhumiwa wa mauaji yake.

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi usiku wa kumakia Oktoba 13, mwaka huu.

Barlow  mwenye Umri wa Miaka 52 aliuawa usiku wa manane eneo la Kitangiri, Wilaya ya  Ilemela, Mkoa wa Mwanza, baada ya kutoka kwenye kikao cha harusi, alipokwenda kumshusha Mwalimu Doroth Moses, aliyekuwa amempa lifti.

Mkuu wa Jeshi la Polisi.IGP Said Mwema, akizungumza  na vyombo la habari amesema polisi inawashikilia watu 10 wakituhumiwa kuhusika na mauaji yake.

IGP  aliwataja  kuwa ni Muganyizi Peter mwenye umri wa miaka (36) aliyemkamatwa Jijini Dar es Salaam kuwa  anadaiwa  kuwa ndiye aliyempiga risasi kamanda Barlow.

Wengine waliokamatwa Jijini Dar Es Salaam  ni Chacha Mwita (50), Majinge Marwa (48), Edward Kusoka( na Bhoke Marwa (42).

 Kwa Mujibu wa IGP Mwema watuhumiwa hao walipatikana an bunduki mbili, ikiwemo Shotgun Greenner iliyokatwa kitako, inyaodaiwa ilitumika katika mauaji hayo.
Walikamatwa pia na silaha aina ya Pump Action na simu ya upepo  ya kamanda Barlow.

Amesema watuhumiwa wengine  waliokamatwa jijini Mwanza ni Mwalimu Doroth(42), Felix Felician (50), Fumo Felician (40), Bahati Lazaro (28) na Amos Bwire Bonge (30).

Kwa mujibu  wa IGP Mwema, watuhumiwa hao wapo katika mtandao wa ujambazi na wamekiri kuhusika katika matukio mengine matatu ya ujambazi Mkoani Mwanza, kabla ya wenzao kukimbilia Jijini Dar es Salaam, baada ya mauaji ya Kamanda Barlow kufanyika.

IGP SAID MWEMA, amesema kukamatwa kwa watuhumiwa  hao ni kunatokana na simu ya Mwalimu Doroth waliyokuwa wakitumia baada ya mauaji.

Watuhumiwa wawili waliokimbia Jijini Dar wanasakwa.

Hongera jeshi la polisi kwa kazi nzuri mliyoifanya, pia hongera TCRA kwa ufuatiliaji kwa njia mtandao.

Vitendo hivi vithibitiwe si kwa kamanda tu bali kwa mauji mengine ya raia pia.

No comments:

Post a Comment