MWENYEKITI WA CCM,Rais Jakaya Kikwete amecharuka baada na kushangazwa na baadhi ya vitendo vya wajumbe vya kutaka kupigana hadharani baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa UWT uliofanyika katika Ukumbi wa J.K NYERERE,Chuo cha mipango.
Rais kikwete pia alionekana kukerwa na kauli za baadhi ya wagombea kudai kuwa wanatetea kiti .
Alisema kuwa hakuna Mwenye kiti chake bali kila mwanachama anapaswa kugombea nafasi yoyote katika Chama.
Alizungumzia juu ya fujo zilizokuwa zikitaka kufanyika katika Ukumbi huo baina ya Mbunge wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji na Sofia Simba katika Ukumbi huo alishangazwa na kitendo hicho na kwamba hakutegemea kina mama kufanya kitendo hicho cha fedheha na kinachoonyesha kutokomaa kwa wanachama wake.
'Kama wewe unajua unaweza kwa nini uweke mambo yasiyo na maana, nenda shule kasome usionee wengine,hakuna kiti cha mtu hapa kila mwanachama ana haki ya kuchukua fomu na kuomba nafasi yoyote anayoitaka kwa nini uwe na mashaka kama wewe ni mkomavu?alihoji Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika ufungaji wa Baraza la UWT Taifa huku akishangiliwa na wapambe wa Anne Kilango Malecela.
Mara baada ya hotuba kali ya RAIS wapambe wa ANNE KILANGO MALECELA walionekana kufurahi huku kila mmoja kipiga simu mikoani na kusema kuwa 'kwa kweli tuna amani kubwa, RAIS amezungumza,amesema sana,kwa kweli hotuba hii ingekuja jana,tungeshinda katika uchaguzi huu,alisikika Mjumbe Mmoja akizungumza na wana UWT kwa njia ya simu.
JK aliendelea kusema Chama kinapokwenda sipo,kama unataka madaraka kwa rushwa wewe si kiongozi,UWT ni jeshi kubwa,na Maana yake ni kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwa huru na haki pia maana ya UWT na Kwa mujibu wa katiba ya TANU akinukuu alisema Dhana ya TANU ni kuhakiksiha Chama kinashinda katika chaguzi zote kuanzia Kitongoji,hadi Taifa na lazima tuangalie 2015 Kinashika dola kuanzia nafasi zote.
'Ni vitu vya ajabu sana vinafanyika kwa upande wa NEC walikuwa wamekata majina ya watu, kwa nini uwakata waache wakashinde wenyewe ukumbini , mkifanya hivi kutakuwa na hatari mbele ya safari,watasema aah!!! Chama kina wenyewe....wenyewe yeye atakuwa hayumo ni hatari sana! alisema JK.
Mara baada ya hotuba hiyo, Rais Kikwete aliwakaribisha wajumbe hao kupata chakula cha Usiku na kuagana nao kwa kuwatakia safari njema na kufanya kazi kwa bidii ili CCM iendelee kuongoza dola.
Wajumbe hao wameondoka leo alfajiri kuelekea Mikoani,huku nyumba za kulala wageni zikipokea wajumbe VIJANA,na maisha yakiendelea kuwa magumu kutokana na uhada wa chakula,kupanda bei kwa baadhi aya vyakula na hivyo kufanya wakazi wa Mjini Dodoma kuambulia mboga za majani na nyama ikiwa
Amewataka walioshindwa katika nyandifa za UNEC wa Wilaya kupitia CCM wawe na subra, na kwamba waendelee kukitumika Chama kwa nguvu zao zote bila kujali.
Umoja wa Vijana kesho utafanya Chaguzi zake kwa nafasi mbalimbali za uongozi, huku wajumbe kutoka Mikoa mbalimbali wakiwasili.
Wajumbe kutoka Mkoa wa Mara, Kigoma na Mbeya tayari wameishawasili na maandalizi ya malazi yameifanyika,huku shamra shamra kutoka bendi ya Vijana jazz ikitumbuiza katika Makao Makuu ya Chama Mjini Dodoma ambapo pia ni Makao Makuu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment