Sunday, October 14, 2012

MTOTO WA BABA WA TAIFA ASHINDWA KITI CHA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA.

MUSOMA



MGOMBEA wa nafasi ya kiti, Christopher Sanya Mkoa amepata ushindi wa
kishindo katika kinyangang'anyiro hicho baada ya kupata kura 481 kati
ya kura 912 zilizopigwa  na moja kuharibika na kumshinda Makongoro
Nyerere  mgombea mwenzake aliyekuwa akitetea nafasi  hiyo kwa kura 59
baada ya kurudiwa uchaguzi.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi mkuu ambaye ni mjumbe wa
halmashauri kuu CCM Taifa kutoka Bukoba Nazir Karamagi alimtangaza
Makongoro kuwa amepata kura 422.

Katika matokeo ya awali msimamizi huyo alisema Christopher Sanya
alipata kura 469,Makongoro Nyerere kura 402 na Enock Chambiri kura 144
kati ya kura 1012 zilizopigwa na moja kuharibika ambapo kura hizo za
wagombea hazikuvuka nusu hali ambayo ilisababisha upigaji wa kura hizo
kurudiwa.

Makongoro alikubaliana na matokeo ya ushindi huo ambapo alimuasa
mshindi wa nafasi ya uenyekiti mkoa Sanya kufanya kazi kwa mujibu wa
katiba ya chama na kuvunja makundi yaliyoshamili ndani ya chama kwani
na yeye ni mmoja wapo wa viongozi wa mkoa na hivyo atahitaji
ushirikiano wake katika kukiongoza chama.

"Naomba uwe muadilifu, mkoa huu wa Mara ni mgumu sana kuufanyia
kazi,kwani kazi ya uenyekiti siyo lelemama, hii ndiyo nafasi kubwa
ambayo itatusaidia katika uchaguzi wa 2014-2015".alisema Makongoro.

"Wewe ndiye kiongozi mkuu wa mkoa huu wa kupanga uongozi katika
uchaguzi mkuu hivyo ukishindwa tutayumba tunaomba utoe ushirikiano na
kwamba dhambi ya kukata majina itaingia kwenye ngazi ya serikali za
mitaa"aliongeza.

Aliwataka pia wajumbe kuachana na mambo ya kambi na kwamba uchaguzi
umekwisha kilichopo ni kushikamana na kuwapa ushirikiano viongozi
waliochaguli ili wakiongoze chama vizuri na kukiandaa katika uchaguzi
mkuu.

Katika nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa kila wilaya nafasi
mbilimbili kwenye mabano kura zaoJosephat Seronga (621) na Ester
Nyarobi (567) katika wilaya ya Serengeti, Zuhura Makongoro(455) na
Jackson Waryoba (307) wilaya ya Bunda , Josehat Kisusi (450) Felister
Nyambaya (421) wilaya ya Rorya.

Wengine ni katika wilaya ya Butiama ambao,Grace Bunyinyiga (494) na
Thabita Idd (381),Abdalah Jumapili (462) na Hamisi Kananda (411)
wilaya Musoma mjini na katika wilaya ya Tarime Mariam Mkono (744) na
Samson Gesase (598)

No comments:

Post a Comment