Sunday, October 7, 2012

MAKONGORO NYERERE ASIKITISHWA NA WAJUMBE KUDAI POSHO CCM (MARA)

MUSOMA.



MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara nayemaliza muda wake,  Makongoro Nyerere  amesema kuwa jambo la posho ni jambo jema kwa wanachama lakini limeingia vibaya ndani ya chama kwani limefanya wajumbe kutochagua kiongozi bora na kujali wenye fedha zao.

Akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya  kwenye kikao cha kwanza cha tathmini za uchaguzi uliofanyika kilichofanyika hivi karibuni alilalamika jambo la posho.


“Posho ni jambo jema lakini limeingia vibaya katika CCM limefanya watu wetu kusema kuwa kama hutoi posho hutakiwi kuonekana  sura yako.”Alisisitiza Makongoro.

‘Tatizo chama chetu hakina mradi wowote  wa kuzalisha tunapaswa tutafute mradi ili tuweze kujiwekea akiba tunapota shughuli mbalimbali kama hizi ziweze kutusaidia badala ya kutegemea mgombea kuja kuwawezesha wajumbe.”,aliongeza.

Makongoro alisema  kuwa kila mjumbe anayo haki ya kulipwa posho kama wanavyolipwa wajumbe wa Kitaifa kwani bila wao wajumbeo hao wa kitaifa wasingekuwepo.

Alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama ambao hawana fedha na wenye fedha hawapewie nafasi  bila kwa sababu zisizo  za msingi.

Makongoro Nyerere aliowaomba wajumbe hao waweze kumpigia kura katika uchaguzi utakaofayika oktoba 13 mwaka huu .

Wagombbea katika nafasi hiyo ni  Enock Chambiri na Christopher Sanya.

No comments:

Post a Comment