MBUNG E wa Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji amebwagwa katika kinyang’anyiro cha Ujumbe Baraza Kuu la UWT Taifa, kuwakilisha kina Mama kutoka Mkoa wa Mara baada ya kushindwa na mjasiliamali mdogo, Agness Mathew alipata kura 274.
Shy-Rose ambaye pia ni
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Jamii Benki ya NMB alipata kura 249,
kati ya kura 526 zilizopigwa.
Awali akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi, Jackson
Msome alisema alimtangaza Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mara kuwa ni Nancy Msafiri
alipata kura za ndiyo 429 na kura 89 za hapana.
Aliwangaza wengine katika nafasi na kura zao zikiwa kwenye
mabano kwa ya Mjumbe Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa, alipata Stellah Manyonyi(312),
Mkutano Mkuu CCM Taifa, Amina Masenza aliyepata kura (273), na nafasi ya kuwakilisha Wazazi Mkoa, Mercy
Mollel alipata kura 195 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Rose Magoti, ambaye
pia ni diwani wa viti Maalum (145),.
Nafasi ya uwakilishi vijana ilikwenda kwa Victoria Chacha (271) na kumshinda Lina Lucas
aliyepata kura (97) na katika nafasi mbili mbili kila Wilaya za Ujumbe wa
Baraza la UWT Mkoa waliopita bila kupigwa kutoka Wilaya ya Bunda ni Chausiku Luzama na Salome Lutoryo, Wilaya
ya Rorya ni Marimu Odunga na Tamary Nashon
Waliopigiwa kura katika nafasi hiyo kutoka Wilaya ya
Serengeti ni Maria Chacha(228) na Dorice
Kiraryo(129), katika Wilaya ya Butiama walioshinda ni Yustina Ngega(294) na
Anna Bianda (186), Wilaya ya Tarime Kichena Chambiri alipigiwa kura akiwa
amelazwa hospitalini baada ya kupat ajali akiwa njiani kuelekea kwenye uchaguzi
huo kwa kupata kura (321) na Justina Mantago (245).
Awali akifungua kikao hicho cha Uchaguzi Mlezi wa UWT Mkoa
wa Mara, Christopher Gachuma aliwaasa wachague viongozi walio bora na
watakiokijengea Chama uwezo kwa kushinda katika uchaguzi ujao wa ngazi za
vitongoji hadi Taifa.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa UWT
Mkoa, Nancy Msafiri aliwataka wabunge wa viti Maalumu kushiriki kikamilifu
kuhakikisha wanashiriki katika Chaguzi zote.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome alitumia fursa
hiyo kuomba kura kwa wajumbe kutoka Mkoa wa Mara watakamchagua Mjini Dodoma
NEC ya watu 10 kutoka Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment