MRADI WA MAJI WEGERO WACHAKACHULIWA.
BUTIAMA/SERENGETI
MRADI wa Maji Wegero
ulioko katika Wilaya ya Butiama unaolalamikia na wananchi sasa kupata ufumbuzi.
Mradi huo uliogharimu
jumla ya Sh.Milioni 969 .9 ulikabidhiwa kwa halmashauri ya Musoma Vijijini
Feb.27 mwaka huu ambapo mkandarasi wake alikuwa kampuni ya Mwanza ya Jassie ya
Jijini Mwanza.
Akizungumza mara baada ya
kukagua bwawa hilo, Naibu Waziri wa Maji, Dk.
Eng. Binilith Mahenge alisema ataleta wataalamu kuhakikisha ubora wa ujenzi wa
bwawa hilo na kwamba tayari amemwagiza
Mkandarasi aliyejenga bwawa hilo
kurekebisha mapungufu yaliyopo.
Akijibu hoja mbalimbali
zilizoulizwa na wakazi wa kijiji hicho juu ya kutumia maji hayo kwa kuwa bwawa hilo halijakabidhiwa
rasmi, alisema wananchi waendelee kuyatumia kwani hayana madhara yoyote.
Ujenzi wa Bwawa la Wegero
lilisimamiwa chini ya Mtaalam Mshauri Kampuni ya Netwas Tanzania Limited ya Jijini Dar
es Salaam ambapo ujenzi wa bwawa hilo ulianza Mei Mosi 2009.
Mbunge wa Jimbo la Musoma
Vijijini, Nimrode Mkono amekuwa akilalamikia ujenzi wa bwawa hilo kuwa halina kiwango na halikupaswa
kukabidhiwa.
No comments:
Post a Comment