MUSOMA.
Ziara ya Naibu Waziri wa Maji, Dr.Eng. Binilith Mahenge
imevumbua mengi yakiwemo madeni ya muda mrefu kwa wafanyakazi , wadeni,
uchakavu wa mitambo ya maji Wilaya ya za Musoma na Butiama.
Akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na taka katika ofisi za Mamlaka hiyo Wilaya ya Musoma, wafanyakazi hao walipata
fursa ya kutoa maoni na dukuduku zinazoikabili Mamlaka hiyo.
Akielezea tatizo la ulimbikizwaji wa madeni hasa kwa Taasisi
za Kiserikali, Mhasibu wa (MUWASA) Richard Chisimbili alisema kuwa jeshi la
polisi linadaiwa jumla ya Sh. Milioni 98 ambapo pamoja na kutuma taarifa kwa
IGP Said Mwema deni hilo halijalipwa na kwamba ni la muda mrefu sasa hali
ambayo inasababisha uendeshwaji wa Mamlaka hiyo kuwa mgumu.
Naye Gantala Said alimwelezea Naibu Waziri kuwa makusanyo ya mapato ya maji kwa mwezi ni
Sh.Milioni 105 hadi Milioni 110, malipo
ya gharama za umeme kwa mwezi ni Sh. M.50, mishahara na makato ni Sh.Milioni
46, usomaji mita ni Sh M.6, madawa ya kuweka kwenye maji ni Sh. M. 5 hali ambayo inasababisha watumishi kulipwa
mishahara ama kucheleweshewa mishahara yao hadi kupungua kutoa Sh. M.46 hadi
Sh. M.26.
Akizungumzia upotevu wa maji
katika Manispaa ya Musoma, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo (MUWASA), Genes
Kaduri alisema kuwa Mamlaka inapotez afedha nyingi kutokana na wateja wengi
kutokuwa n a mita za maji, hali ambayo kwa sasa wanalipa kwa kukadilia matumizi
ya mwananchi, pia baadhi ya viwanda kutumia maji ya moja kwa moja kutoka ziwani
bila kulipia kutoka kwenye Mamlaka hiyo.
Akitoa ombi kwa Naibu Waziri, Naye Edson Mwambene alisema
kutokana na tarifu ya umeme kuwa kubwa, aniomba
Wizara kuangalia suala la kuondoa VAT
kwenye umeme na madawa ya maji ili mamlaka hiyo ipate angalau unafuu kidogo.
Akijibu hoja hizo Naibu Waziri alisema kuwa atawasiliana na
wadeni hao ili walipe madeni yao, pia suala la VAT amelipokea na litafanyiwa
kazi.
Naibu Waziri Dr.Eng. Binilith Mahenge alisema kuwa Serikali
tayari imetoa Sh. Milioni 40 kwa ajili ua mradi wa Maji Manispaa ya Musoma na
kutoa wito kwa wafnyakzi na watumishi wafanye jitihada za makusudi ili
kuboresha maji katika Manispaa,kwani maji ya sasa ni machafu kutoka na kuwa na
chujio chakavu,hali ambayo inahatarisha maisha ya wakazi wake.
Akisoma taarifa kwa Naibu Waziri, Meneja Mradi wa Maji, Mugango/Kibakari/Butiama,
Merchades Anaclet alisema kuwa mpaka
mwishoni mwa mwezi Septemba 2012 jeshi
la la wananchi kikosi cha kiabakari(253KJ) linadaiwa jumla ya Sh.57,905,918 za
umeme na mitambo.
Naibu Waziri Mahenge yuko Mkoa Mara kwa ziara ya kutembelea
miradi ya Maji ambapo amekwenda katika mradi wa maji wa
Mugango/Kiabakari/Butiama na amezulu kaburi la Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu
Julius Nyerere na kumsalimia Mjane wa
Mwalimu Maria Nyerere ambaye ambaye aliwasili muda mfupi akitokea Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment