DODOMA.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Halfan Mrisho Kikwete,amefungua Mkutano wa 8 wa Jumuiya ya UVCCM Taifa huku kukiwa na taarifa kuwa mwanawe,Ridhwan Kikwete (MNEC) na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kudaiwa kupanga safu za uongozi.
Mkutano huo wa aina yake umefunguliwa majira ya saa 11:30,huku wajumbe wakitaka kutopangiwa safu za uongozi.
Wakizungumza kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano huo,baadhi ya wajumbe walidai kuwa wamechoshwa kupangiwa safu za uongozi na kwamba watachagua kiongozi wanayeona anafaa na atakayekivusha chama katika harakati ya uchaguzi Mkuu wa 2015.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya kugombea Uongozi katika nafasi ya UNEC imetiafola kutokana na Kamati ya Siasa na Kamati Kuu kupendekeza majina yapatayo 40 huku vikitakiwa viti 6 (Bara),viti vinne Zanzibar wagombea wapo 22.
Kwa upande wa Baraza Kuu vijana Taifa viti vitano(Bara) wagombea wako 39 na viti vitano Zanzibar wagombea wapo 14,Uwakilishi Wazazi Taifa na UWT wagombea 16 kila nafasi.
Nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Taifa wanaochuana ni Lulu Mushamu Abdallah, Sadifu Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka,wakati nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Ally Salum Hapi, Paul Christina Makonda na Mboni Mohamed Mhita.
No comments:
Post a Comment