MUSOMA
ZIWA
Victoria limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Mji wa Musoma kutokana na tatizo
la ukosefu wa maji katika baadhi ya maeneo ya Mji wa Musoma Mkoa wa Mara, ambapo
kwa sasa ni la takribani siku tano.
Uchunguzi
uliofanywa na blog hii, umebaini kuwa wakazi wa maeneo ya kando kando ya ziwa hasa,
Baruti, Bweri na Iringo wamekuwa wakichota maji katika ziwa hilo kutokana na
kukosa maji ya bomba katika maeneo wanayoishi huku njia mbalimbali za boda boda
na baiskeli na vichwa vya akina mama wakibeba
maji hayo kutoka ziwa hilo.
Wakizungumzia
suala hilo kwa nyakati tofauti, Mkazi wa Bweri, Gabriel Kambuga Mkazi wa Kata
ya Bweri, alisema kuwa kwa sasa wana takribani wiki moja hawajapata huduma hiyo
na hivyo kuwalazimu kwenda kuchota ziwani ambapo maji hayo hayana usalama.
Naye mkazi
wa Kigera, Edward Patrick aliyefika katika ofisi za Muwasa kutaka kujua huduma hiyo
itarejea lini,alisema kuwa eneo hilo halijapata maji kwa muda wa wiki
moja,lakini tatizo lao halihusiani na kutatika kwa bomba Mtaa wa Nyerere.
Afisa Mahusiano wa Mamlaka ya Maji safi na Taka Mjini Musoma(MUWASA),
Emmanuel Ruyobya amesema kuwa tatizo
hilo limetokana na upanuzi wa barabara ambapo Kampuni ya Kichina imekata
mabomba ambayo yanasafirisha maji kwenda kwa wakazi sehemu mbalimbali za mji
huo.
“Mabomba
yaliyopo yamechakaa sana, na yana miaka kama 50 hivi, sasa yanapokuwa
yanahamishwa ili kupisha ujenzi wa barabara yanakatika, hilo ndo tatizo kubwa lililosabisha
wakazi hawa kukosa maji,jitihada zinafanywa ili kurejesha huduma hiyo haraka”
Alisema Ruyobya
Maeneo ambayo hayana Maji ni Iringo,
Nyamatare, Mkendo kati, Kigera, Kwangwa, Nyakato, Nyasho, kitaji,Bweri na Kiara.
No comments:
Post a Comment