BUTIAMA
CHAMA cha riadha Mkoa wa Mara, Oktoba 14 mwaka
huu, kilimuenzi Baba wa Taifa,Hayati Mwl.J.K Nyerere kwa kufanya mbio ya Kilometa 21 na ushindi
kupatiwa zawadi.
Akizungumza mara baada ya Mashindano hayo,
Kamishina wa habari na uenezi wa Chama
chama cha riadha Mkoa wa Mara, Eva-Sweet Musiba alisema kuwa Chama kimeamua
kufanya mbio hiyo ili kuenzi mchango wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius
Nyerere katika nchi hii kwa kuleta Uhuru, uzalendo,Amani na Utulivu katika nchi
hii.
“ Tumeamua kuunga mkono jitahada za Mwalimu
Nyerere alizozifanya katika nchi hii, pia kuipenda michezo,hatukutaka kuwa
nyuma kwa michezo ingawaje yeye alikuwa anapenda mchezo wa bao, lakiji sisi
tumeamua kufanya hivyo ili kumkumbuka Baba yetu ambaye alikuwa msitari wa mbele
katika michezo yote” Alisema Musiba.
Pia alitoa shukurani kwa Mgodi wa Dhahabu wa North
Mara Barrick kwa kuchangia gharama za mashindano hayo na kuwataka wawekezaji
wengine, mashirika ya umma, watu binafsi
na Serikali kuunga mkono jitihada za wawekezaji ili kukuza mchezo huo ambao ndio pekee
unalitangaza Taifa hilo kwa wachezaji kuwakilisha Taifa.
Mbio hizo zilizoanza majira ya asubuhi juzi ambapo
Mkuu wa wilaya ya Butiama, Angeline Mabula alizianzisha kwa kupuliza
kipenga,kutoka viwanja vya Joseph
Kizurira Nyerere kuelekea barabara ya Kiabakari na kurudi.
Mbio hizo zilishirikisha wanariadha wapatao 10
kutoka wilaya za Butiama, Musoma Mjini, Rorya na Tarime ambapo washindi wa tano bora walipatiwa zawadi zao za fedha
taslimu.
Mshindi wa Kwanza Majina yao na fedha zikiwa
kwenye mabano ni Mwita Kopilo kutoka Wlaya ya Tarime aliyekimbia 1:05:23 alipewa
Sh. (70,000), Mshindi wa pili Juma Issa Wambura wa Tarime aliyekimbia 1:10: 03
alipata Sh. (50,0000), Mshindi wa tatu,Mukama Magesa kutoka Wilaya ya Butiama 1:13:19
alipata Sh. (30,0000) wa nne na wa tano ,Nyakutonya
Berias wa Wilaya ya Butiama 1:20:47 na Chagembe Maira 1:22:00 walipewa Sh. 25,000 ambapo Mkuu wa
Wilaya Angelina Mabula alikabidhi zawadi hizo.
No comments:
Post a Comment