Friday, April 17, 2015

MILIONI 229 ZAHITAJIKA UKARABATI HOSPITALI YA TARIME.

TARIME-MARA.

MKUU wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga amesema zaidi ya Sh. Milioni 229 zinahitaji kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa hospitali ya Wilaya ya Tarime ambayo inabiliwa na uchakavu wa miundo mbinu ya majengo pamoja na kuwa na uhaba wa madawa,mashuka na vyandaruaili kuondoa tatizo kubwa liliopo kwa sasa linalowakabili wananchi wa Wilaya hiyo na zingine pamoja na nchi jirani ya Kenya ambayo kwa kiwango kikubwa wanapata matibabu katika hospitali hiyo.

Kuhusu suala la madawa amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wa majengo atakikisha upatikanaji wa madawa unakuwa wa kuridisha kuliko ilivyo hivi sasa, hali ambayo imesababisha wananchi kutojiunga na mfuko wa CHF unaowataka kuchangia kiasi cha sh. 10,000 kwa ajili ya kupata huduma hiyo.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya maboresho Peter Zakaria ambaye alichangia Sh Milioni 10 alisema kuwa hatakubaliana na ujinga wowote kwa kwamba anaonea uchungu fedha za umma kuteketea bila kufanya kazi yoyote na kwamba atahakikisha anasimamia vyema ujenzi huo na kwa uadilifu mkubwa.

Katika harambee hiyo iliyoshirikisha watumishi wa Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, Mgodi wa Acacia wa North Mara na watu binafsi jumla ya Sh Milioni 281.4 zilichangwa kupitia Akaunti ya benki ya NMB uboreshaji wa hospitali ya Wilaya ya Tarime N0.30410011011 , mashuka 50, madawa na vyandarua.
Hospitali ya Wilaya ya Tarime ilianzishwa mwaka 1956 ikiwa n alengo la kuhudumia wilaya hiyo na viunga vyake ambapo ilitoa huduma kwa kiwango cha Zahanati lakini kwa sasa idadi ya watu imeongezeka na inahitaji watumishi wengi ili kuweza kuendesha huduma hiyo ipasavyo.





No comments:

Post a Comment