Saturday, May 22, 2010

BODI YA WAKANDARASI

MKUU wa Mkoa wa Mwanza,Abbas Kandoro akifunga Mkutano wa Wakandarasi wa eneo la Maziwa Makuu katika Ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu,jijini Mwanza, Kulia kwake ni Msajili wa Bodi ya Makandari Nchini ,Boniface Muhegi na Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Nchini Charles Kitwanga.
Uharibifu wa Miundo mbinu ya Barabara ulivyofanywa na greda,baada yakatwa kwa mabomba ya maji katika eneo la Mkolani Mtaa wa Uzunguni Wilaya ya Nyamagana.



WAZIRI Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wakandarasi Chuo cha Benki Kuu jijini Mwanza.
WAZIRI NA WAKANDARASI wa Maeneo ya maziwa Makuu.

Tuesday, May 11, 2010

WATANGAZA NIA ZA UBUNGE NA PESA ZAO.

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutia saini Mswada wa sheria ya Uchaguzi Mkuu, Bado kuna vichwa visivyo sikia la Mkuu,ambao pamoja na Rasi kuzungumzi rushwa vichwa hivyo vimekuwa vigumu na vinaendelea kumwaga pesa katika majimbo ambayo vitakwenda kugombea.

Hii ni hatari sana katika nchi yetu yenye demokrasia na vyama vyingi, ambapo
Pamoja na Rais kukemea vikali rushwa wanaendela kuwmaga pesa ili wapewe kura na wanachi ambao hawajua nini cha kufanya aizdi ya kupokea pesa zao.

Kwa bahati mbaya hasa wale walioko vijijini wamekuwa wakipewa pesa hizo maskini ya Mungu bila wao kujua kuwa haki zao zinakwenda bure bila mafanikio yoyote,, na kwa kuzingatia pesa ya muda tu ambayo si chochote wala lolote.

Najuta kusema hili na kusikitika sana kwa kuwaRaisi wetu amekuwa muungwana sana kuhakikisha kuwa hata wasionacho waweza kuongoza na kuliongoza Bunge kwa uadilifu wa hali ya juu na kuwajali masiki kabisa walio na kipato cha chini kwani wafahamu kuwa wao pia walipaya uongozi kwa ridhaa yao.

Sasa hao wanaotoa pesa wanataka nini? na walikuwa wapi kuasidia wanachi wakati ule ambao hawakuwa nacho.Tatizo za viongozi wetu nikiwemo na mie ambaye hivi karibuni nitatangaza rasmi nia hukju mjini Musoma,Tusiwashau na tusijishau kurudi majimboni tupatapo uongozi, ili tuweze kuwasidia wenzetu ambao waliotupatia ridhaa ya kuingia madarakani.

KIKAO CHA GHAFLA CHA MADIWANI CHAITISHWA MWANZA.

Kikao cha Baraza la dharula cha baraza la madiwani Jijini Mwanza kimeitishwa leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wilson Kabwe kwa njia ya Simu kwa waandishi wa habari ni cha ghafla sana ambacho kinaweza kuwa na ajenda kali za madiwani wa jiji hilo.

Kikao hicho kibnatajia kuanza mchana huu katika Ukumbi wa mikutano wa Jiji la Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa kutoak amkwa baadhi ya wadau wa habri Mkoani hapa inasemekana kuwa kunaweza kuwa na ugomvi katia ya madiwani ama kuanza kwa kampeni zisizo rasmi kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ilisainiwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk Jakaya Kikwete.