Tuesday, May 3, 2011

HABARI NA GHATI MSAMBA
MUSOMA.

VIONGOZI wa Mkoa wa Mara wamepata mafunzo juu ya utekelezaji wa sera na sheria ya ardhi ya vijiji ya namba 5 ya mwaka 1999.

Akitoa maelekezo ya sheria hiyo katika semina ya siku mbili ya mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji wa mkoa wa Mara Naibu katibu mkuu wa Wizara ya ardhi Maria Bilia alisema kuwa lengo ni kuelimisha wananchi na wataaalamu juu ya utekelezaji wa sheria ya asrdhi ya vijiji waweze kupata fursa ya kuchangia na kutoa changamoto zinazojitokeza katika masuala mbalimbali ya migogoro ya ardhi mkoani hapa.

Alisema kuwa katika kutekeleza sera hiyo ya umilikishwaji wa ardhi vijijini wananchi wawe na uwezo wa kupata cheti cha ardhi na kila kijiji kuwa na daftali la kijiji ili kubainisha ardhi inayopmilikiwa na kupima mipaka ya kila kijij Tanzania Bara hatua kwa hatua.

“Ni muhimu kuelewa kuwa ili hati za haki miliki za kimila zianze kutolewa shart kwanza ziwepo masjala za ardhi katika ngazi ya Wilaya na kijiji,kijiji husika kiwe na cheti za ardhi ya kijijimambacho ndicho kinachotoa mamlaka kwa halmashauru ya kijiji katika kusimamia ardhi ya kijiji kwa mujibu wa sheria”alisema Bilia.

Alisema kuwa Wizara ya nyumba na maendeleo na makazi ilianza kuhamasisha na kuwezesha mikoa na wilaya ili kuanza utekelezaji katika vijiji ili umilikaji wa ardhi kimila vijijini kurasimisha ardhi kuwa mtaji hai ambapo wamiliki wa ardhi wapewe hatia za kumiliki ardhi kimila na kuborsha usalama wa kumiliki ardhi zao.

Aliongeza kuwa hali hiyo itafanya wananchi kuwa na uwezo wa kupata fursa na dhamana ya kutumia hati hizo katika vyombo vya fedha ,mahakamani na hata kusomesha watoto wao katika vyuo vikuu vya elimu ya juu.

“Miongozo mbalimbali ya Serikali na chama tawala inahimiza matumizi bora yanardhi ili kuondoa umaikini na kuongeza uwezo wa serikali kutambua kisheria miliki mbalimbali zaardhi na katika uchumi wa kisasa haitoshi kuwa na haki ya kutumia ardhi bila miliki hiyo kutambuliwa kisheria”alisema Naibu katibu huyo.

Bilia alisema kuwa Wazara inaendelea kupanua wigo wa utekelezaji kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu kwa uuma na kuboresha usalama wa miliki na matumizi bora ya ardhi na kuratibu uasisi na uanzishwaji wa masjala za ardhi za wilaya na vijiji na utoaji w vyeti vya ardhi,pamoja na hati miliki za kimila kwa wananchi.

Naye Kaimu kamishna msaidizi usimamizi wa ardhi vijijini Suma Mbyopyo malisema kuwa matatizo yaliyosababisha kutungwa kwa sera ya Taifa ya ardhi ni pamoja na idadi ya watu kuongezeka na mifugo,ongezeko la mahitaji ya matumizi ya ardhi ,mashamba,maeneo ya malisho ya mifugo mwamko wa watu kutambua umuhimu wa ardh na uharibfu wa mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya tarime John Henjewele ambaye alikuwa mwenyekti wa semina hiyo aliwataka viongozi na wataalam kutumia mafunzo hayo katika kutatua migogoro ya ardhi ambayo ni kikwazo kikubwa mkoani humo .

“kutokana na kutotolewa kwa sheria hizi za ardhi kumeendeleza kuwpo kwa migogoro ya mara kwa mara na kusababisha mapigano ya koo na koo kutoelewana kwani ardhi ni rasilimali mama hivyo itabaki kuwa msingi bora katika kuleta maendeleo yetu”alisema Henjewele.

No comments:

Post a Comment