MUSOMA.
MSTAHIMIKI Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura,amemshambulia Mama yake kwa kumchapa kwa viboko kwa kutumia fimbo maeneo ya makalio,Mgongoni na sehemu nyingine za mwili wake kwa kosa la kukutwa na watu wa jinsia ya kiume ambao hawakufamika majina na mahusiano yao.
Akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari Mama wa meya huyo,Scholastika Malima alisema tukio hilo lilifanyika Aprili 26 mwaka huu (Jumanne) majira ya saa 1.30 usiku nyumbani kwake mtaa wa Nyamatare Mjini Musoma.
Alisema kuwa kisurura alimkuta na wanaume wakiwa wamekaa na mama yake na kumwuliza kwanini anapeleka wanaume katika nyumba hiyo wakati aliishamuzuia na alipomjibu kuwa hawa wameniletea simu ili aione kama inafaa kwa kuinunua ndipo alipochukua fagio na kumtumia na kuchukua fimbo na kuanza kumpiga nayo.
Kwa mujibu wa Mama Malima alisema kuwa purukushani hizo zilisaidiwa na wanae wawili wa kiume ambao hata hivyo hakutaka kutaja majina yao, na kufanya maamuzi ya kwenda kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mara Sekondari,Julius Manyori ambaye alichukua hatua kwa mujibu wa sheria ya kuandika barua kwenda kituo cha polisi,barua ya tarehe 27.4.2011 ambayo haina kumbukumbu namba lakini ina muhuri.
“Lakini baada ya kuwasiliana na simu na Mwanangu aishiye mkoani Arusha alinishauri niesinde kituoni na badala yake tuzungumze na tuyamalize kifamilia.’’alisema mama huyo.
“Nashangaa huyu Meya amekuwa akinisumbua sumbua mara kwa mara lakini sijawahi kumchukulia hatua yoyote kutokana na kutokuwepo ushahidi lakini kwa siku hiyo aliyonipiga walikuwepo wanangu wawili wa kuzaa”,Aliongeza.
Alidai kuwa yeye alishazoa kukaa na watu kutokana na umaarufu wa mumewe wakati alipokuwa akifanya kazi ya uhakimu wakati wa uhai wake na kwamba yeye vile vile alikuwa akifanya kazi ya ualimu.
Licha ya hayo mama kisurura alisema wanamsubiri Meya aweze kurudi kutoka safari ili waweze kutatua kifamilia pamoja na kumlipa pesa zake za matibabu.
Mwenyekiti wa Mtaa Julius Manyori, ambaye pia alihojiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari endapo madai hayo aliyafikisha kwake alikiri kuwa Mama huyo alikwenda kutoa malalamiko hayo kwake na ndipo alipomwandikia barua kwa kuwa kesi hiyo ni ya jinai.
“Nilimwambae aende kituo cha polisi ili apewe hati ya matibabu(PF3),kwa mujibu wa sheria ,lakini sijui amefikia wapi,kwani kazi yangu niliishaifanya”Alisema Manyori
Jitihada za kumpata Msitahimiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex kisurura kuzungumzia suala hili alikata na kuizima simu yake ya mkononi baada tu aliposikia utmbulisho wa kuwa ni waandishi wa habari.
Alisema kuwa Meya kisurura ni mwanae aliyemlea wakati alipoolewa na baba yake yaani mumewe aitwaye Kisurura ambaye kwa sasa ni marehemu ambaye amemlea akiwa mdogo hadi sasa ambapo anaishi nae.
No comments:
Post a Comment