Monday, February 10, 2014
Askari polisi wawili mahututi
ASKARI POLISI wapatao tisa wamejeruhiwa na kati ya hao wawili hali
zao si nzuri,wakati wanashughulikia tukio la ajali ya Bus la Super
Samy lenye namba za usajili T227 CDV,ambalo linafanya safari zake
kutoka Mwanza-Musoma, iliyomgonga mwendesha pikipiki Desderi Charles
ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Kiabakari na kufa papo hapo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Paulo Kasabago (ACP) amesema kuwa mnamo februari 9 katika kijiji cha Songoma Wilaya ya Butiama barabara ya Musoma-Mwanza Mkoa wa Mara,gari yenye namba za usajili T427 BB6 Mitsubishi Fuso mali ya Kisuka
Igogwe Mkazi wa kiabakari likiendeshwa na Garusi Onyango iligonga gari
la polisi PT.1499 L/Rover Defender mali ya RPC Mwanza.
Kabla ya tukio hilo kuwapata askari hao gari hilo lilikuwa likitokea
Wilaya ya Tarime kuelekea Mwanza ambapo lilikuwa limeegeshwa huku
askari wakiwa wanashughulikia tukio la ajali ya bus hilo ambapo
marehemu alikuwa anatoka shule jirani kuwasalimia wanae na alikuwa
amepanda pikipiki yenye namba za usajili T622 AUS.
Askari hao ni D.2216 RSMJohn, E.212 CPL Esore Mwita, H.3532 PC Dominic
Michael, G.6862 PC Erick, G.5112 PC Emmanuel, G.5900 PC Sebastian,
G.7087 PC Thomas, na G.2227 PC Musa na G.3212 PC Elikana.
Katika tukio hilo watembea kwa miguu wapatao wawili waliokuwa eneo la
tukio waligogwa na kupata majeraha, amewataja kuwa ni Jumanne
Abdalah(39) mkazi wa Butiama na Emmanuel Kubunja (30) mkazi wa Bunda
na wote wamelazwa katika hospitali ya Serikali.
Jeshi la polisi linamtafuta dereva wa Fuso ambaye ametoroka baada ya
ajali hiyo na linamshikilia dereva wa Bus kwa mahojiano ambapo mwili wa
marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Serikali Musoma.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara anatoa wito kwa madereva
kuzingatia sheria za usalama barabarani wakati wanapokuwa wanaendesha
vyombo vya moto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment