Saturday, February 8, 2014
Auawa akipambana na Polisi.
MTU mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa na askari polisi katika kijiji cha Nyabisarye Kata ya Bweri Wilaya ya Musoma,majira ya saa moja asubuhi baada ya kupambana na askari akiwa ni SMG moja iliyofutwa namba na imekatwa kitako na mtutu, Marwa Keryoba mwenye umri kati ya miaka 30 na 38 Mkazi wa Kebeyo Sirari.
Marehemu alipigwa risasi baada ya askari polisi kumtaka ajisalimishe ambapo walipiga risasi hewani na kukaidi amri ya askari hao na kuanza kukimbia huku akiwa amebeba silaha hiyo huku akiwarushia risasi, ambapo alifia njiani akiwa anapelekwa hospitali ya Mkoa kwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ferdinand Mtui ikitokea kanda Maalumu ya Tarime na Rorya inasema kuwa katika upekuzi nyumbani kwa marehemu vilipatikana vitu mbalimbali vikiwemo simu za mkononi, CD 2 za picha mbalimbali, deki moja, viatu doti mbili, tochi mbili na mipira ya baiskeli pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani.
Marehemu aliuawa kutokana na taarifa zilizopatikana toka kwa mtuhumiwa mwenzake anayeitwa Charles Range au Kichune au Josephat Chacha au Chalres Josephat Msong’o( 38) Mkazi wa Kenyamanyori Kata ya Turwa Wilaya ya Tarime aliyekamatwa tarehe 6/2/ 2014 Mkoani Tanga.
Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kujihusisha na mauaji na unyanga’nyi wa kutumia silaha yaliyotokea Wilaya ya Tarime kuanzia Jan 25-27 mwaka huu na katika mahojiano na polisi mtuhumiwa huyo anakiri kuhusika na matukio hayo pamoja na wenzake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya, Justus Kamugisha ametoa shukrani kwa wananchi wa Wilaya ya Tarime na Rorya, Mkoa ya Mara na Tanga kwa ushirikiano katika kuwezesha kukamatwa kwa watahumiwa hao na jeshi hilo litatoa zawadi ya Sh. Milioni moja kwa atakayetoa taarifa za mtu anayemiliki silaha kinyume na sheria.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za wahalifu ili kuendelea kuweka Mji wa Tarime na Musoma kuwa salama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment