Monday, February 10, 2014




MADUKA zaidi ya 1000 katika Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara, yamefungwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mgomo baridi unaotokana na kuletwa kwa mashine ya lisiti kwa ajili ya kutoza kodi (EFD) na ambazo zinadaiwa kuwa ni za gharama kubwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mjumbe wa bodi ya wafanyabiashara Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara,Yusuph Kyenche,anasema kuwa mgomo huo utafanyika kwa muda wa siku tatu na endapo hakutakuwa na mwafaka kwa kukaa meza ya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tuppa watagoma kwa mwezi mzima.


Maduka yaliyofugwa ni pamoja na yaliyoko Mjini Musoma, Kamnyonge, Nyasho, Bweri na Makoko yakiwemo maduka ya dawa muhimu ambayo yanatoa huduma za matibabu lakini upande wa soko kuu la chakula la Manispaa likiwa wazi huku wananchi wakiendelea kupata huduma za vyakula.

Akizungumza na wafanyabiashara hao katika bustani ya Malkia Elizabeth, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Tuppa amewataka wafanyabiashara hao kukaa pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mara ili kufikia mwafaka.

Baada ya kumaliza kwa kikao hicho viongozi wa wafanyabiashara hao walikaa pamoja na kuchagua viongozi watakaokwenda kuzungumza na Mkuu wa Mkoa na maafisa wa TRA.
Akizungumzia kuhusu usalama wa Mji endapo kutatokea fujo, Kamishina Msadizi wa polisi (ACP) Paulo Kasabago alisema hali ya usalama mpaka sasa ni shwari, na kwamba jeshi hilo limejipange kukabiliana na vurugu zozote zitakazofanyika.


“Sisi tuko imara, ukiwalazimisha ndo utaleta tatizo lakini kama wao wanaona hiyo ni njia bora kufanya hivyo ni sawa wafanye tu mpaka siku watakayoamua kufungua na hakuna atakayewalazimsha kufungua maduka kwa nguvu,tutateseka ila si busara kwa nini tujitese,Alisema Kasabago.



1 comment: